2016-01-13 14:50:00

Vatican yasikitishwa shambulio la Kigaidi la Uturuki


Baba Mtakatifu Francisko mwishoni mwa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliofika kumsikiliza mjini Vatican Jumatano hii, aliikamilisha katekesi hiyo kwa kutoa mwaliko kwa watu wote, kukumbuka kuwaombea kafara wa shambulio la Kigaidi lililotokea mapema Jumanne mjini Istanbul Uturuki. Shambulio la kigaidi lililofanywa na mtu aliyejilipua kwa bomu na kusababisha watalii kumi kupoteza maisha, kati yao wakiwa wajeruman wanane.  

Mwaliko wa Papa uliombea roho za Marehemu huruma ya Mungu na pia familia za marehemu na wote walioguswa wapate kufarijiwa na huruma ya Mungu.  Bwana wa Huruma, awapokee Marehemu katika amani yake ya milele. Na  pia aliomba mshikamano na umoja imara wa jamii nzima, kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika mioyo yenye kukumbatia njia ya vurugu na ghasia, ili watu hao wachague kutembea katika barabara ya upendo, amani na utulivu katika jamii.

Aidha siku ya Jumanne Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Palon,  alionyesha kusikitishwa na kilichotokea Uturuki , akisema  kilichotokea ni msiba uliogusa watu wote wema  duniani.  Na alirudia kutaja dawa iliyobora zaidi kukomesha unyama huo, ni daima kuwa na moyo wa huruma hata kwa wale wanaofanya unyama huo.

Kwa  mujibu wa taarifa tokea Istanbul watu 10 waliuawa katika shambulio  hilo lililofanyika siku ya Jumanne asubuhi, wilayani   Sultanahmet Istanbul,  karibu na msikiti maarufu unaopendwa kutembelewa na watalii kutokana na historia ya msikiti huo.  








All the contents on this site are copyrighted ©.