2016-01-13 12:11:00

Katekesi ya Papa kwa mahujaji na wageni - Mungu ni Huruma


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano hii katika Katekesi yake ametoa ufafanuzi zaidi juu ya Huruma ya Mungu, Mada inayoongoza  kipindi hiki cha Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Kuomba Huruma ya Mungu.  Mafundisho ya Papa yametazama kwa makini, Huruma ya Mungu kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Biblia. Asema, kwa namna hiyo,  tunaweza kujifunza juu ya huruma ya Mungu  kupitia Neno lake.  Na alianza kutazama maandiko ya Agano la Kale, akisema  Agano la Kale, ni maandalizi  yanayo  tuongoza  katika  kuuona ufunuo kamili wa Yesu Kristo, ambaye ni ukalimifu wa huruma ya Mungu Baba.

Baba Matakatifu ameendelea kusema,  Maandiko Matakatifu,  yanamdhirisha Yesu Kristo kwamba ni Bwana, na huruma ya Mungu. Na hilo ndilo jina lake, analolionyesha katika njia yake kwa sura yake kama tunavyosoma katika kitabu cha Kitabu cha Kutoka, apojifunua  kwa  Musa, kwamba Yeye ni Bwana, na ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.  Papa aliendelea kutaja maandiko mengine yenye kuoneysha huruma ya Mungu ambamo pia mnasisitiza juu ya huruma na upendo wake usiochoka kusamehe (Mwa 4.2; Joel 2:13; Zab 86.15 ; 103.8; 145.8; Ne 9:17). Na ameelezea "huruma" kwamba ni neno  linaloleta hisia za kuiona huruma kama ile ya mama mbele ya mtoto wake,  pia akilitaja neno hili lililotumiwa katika lugha ya Kiebrania katika Biblia, kwamba, humzamisha mtu katika kuwa na fikira za kina zaid, zenye kuionyesha sura ya Mungu katika kuwajali binadamu, kama inavyokuwa kwa mama mwema ambaye hujali watoto wake tangu wakati anapotunga mimba  na huendelea kuwa msaada kwa watoto wake hata anapozaliwa, akiwa tayari kutoa kila kitu alichonacho  kwa upendo mkuu .

Na kwamba, Mungu huyu wa Huruma anayetajwa, si mwepesi wa hasira, bali ni Uvumilivu na Subira, mwenye kujua  wakati wake unaoona unafaa kuingilia kati, si katika haraka za kibindamu , lakini utulivu kama ilivyo kwa mkulima mwenye busara,  anavyosubiri kwa utulivu, mbegu aliyopanda ikote kukua nakutoa matunda mazuri yeliyokomaa. Huruhusu mbegu nzuri aliyonda kukua sabamba na Magugu .

Papa , aliendelea kuafanua juu ya  ukuu wa upendo na uaminifu wa Mungu,  akisema , hapo ndipo kuna uzuri wote, ambapo tunaona licha ya Ukuu na uweza wake wote,  bado anajifunua kwetu kupitia njia ya upendo  na unyenyekevu kwetu sisi ulio wadogo sana na  tusiokuwa na uwezo wowote. . Na kwamba Neno Upendo, linatumika hapa katika maana ya huruma , neema na wema. Papa ameutaja upendo kwamba unpaswa kuwa hatua ya kwanza katika mapito ya binadamu. Na kwamba kuwa na upendo hakuutegemei sifa za kibindamu lakini hutolewa kama  zawadi  ya  bure na Mungu . Ni utendaji wa Mungu ambao hakuna kinachoweza  kuusitisha. Upendo hutolewa hata dhambi, kwa sababu Mungu anajua njia zake za kuwafikia hata wakosefu, kwa kuwa Yeye hushinda ubaya kwa msamaha. 

Papa anasema ni uaminifu usiokuwa na mipaka, kama ilivyofunuliwa katika Neno la Mungu, wakati Mungu anajifunua kwa Musa. Na kwamba Uaminifu wa Mungu haupungui  kwa kuwa Bwana , ndiye nguzo ya upendo huo, kama zaburi anavyosema, halali usingizi lakini huendelea kutuongoza katika njia ya kuelekea maisha ya milele.

Papa alikamilisha Katekesi yake akisema, Mungu ni ukamilifu wa uaminifu wote na uezo imara ulio mbele yetu . Na hiyo ndiyo imani yetu. Papa aliomba katika Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Huruma Mungu, na tujikabidhi kikamilifu katika uaminifu wake, kwa ajili ya kuionja furaha ya kuwa mpendwa wa  katika  Huruma na msamaha wake, Mungu asiyekuwa mwepeisi wa hasira,  lakini mwingi wa upendo na aminifu.








All the contents on this site are copyrighted ©.