2016-01-06 15:24:00

Salam na matashi mema kwa Siku kuu ya Noeli kwa Kanisa la Mashariki 2016


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Tokeo la Bwana, Jumatano tarehe 6 Januari 2015, ameonesha mshikamano wake wa karibu katika maisha ya kiroho na Wakristo wa Kanisa la Kiorthodox la Mashariki wanaoadhimisha Siku kuu ya Noeli, Alhamisi, tarehe 7 Januari 2016. Baba Mtakatifu anawatakia waamini wote hawa amani, ustawi na maendeleo.

Baba Mtakatifu anakumbusha kwamba, Siku kuuya Tokeo la Bwana pia ni Siku ya Utoto Mtakatifu, sherehe inayowagusa kwa namna ya pekee watoto kutoka sehemu mbali mbali za dunia; ambao kwa njia ya sala na sadaka yao, wanawasaidia watoto wenzao wanaoteseka na kuogelea katika mazingira magumu na hatarishi na kwa njia hii wanakuwa kweli ni wamissionari na mashuhuda wa udugu na mshikamano wa dhati.

Baba Mtakatifu ametumia nafasi hii kuwatakia heri na baraka waamini na mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia waliofika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ili kuungana pamoja naye katika kuadhimisha Siku kuu ya Tokeo la Bwana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.