2015-12-28 14:44:00

Tangazo: Padre Dhiya Azzizi OFM. Paroko wa Yacoubieh Syria hajulikani alipo


Shirika la Ulinzi wa Mambo ya Kikristo katika Nchi Takatifu, limetangaza  tangu asubuhi ya  Desemba 23, limepoteza mawasiliano na Padre  Dhiya Azziz OFM, Paroko wa Yacoubieh (Syria). Mawasiliano ya mara mwisho  na Padre Dhiya ni wakati alipokuwa akisafiri kwa teksi , ambamo ndani yake pia kulikuwa na abiria wengine. Padre huyo alikuwa akitokea Lattakia mapema asubuhi  akielekea  katika Parokia yake ya Yacoubieh kwa ajili ya maadhimisho ya Sikukuu ya Noel katika Parokia hiyo,lakini hajawahi kuonekana hadi leo katika Parokia hiyo. .Na kwamba ametoweka wakati akirejea tokea  Uturuki, ambapo alikuwa amekwenda kutembelea familia yake ambao kwa sasa inaishi kama wakimbizi baada Daesh (ISIS) kuingia Karakosh (Iraq), mji wa asili kwa familia hiyo.

Na kwamba,mawasiliano yake kwa njia ya simu yalisajiliwa tarehe 23 Desemba majira ya saa tatu za asubuhi na tangu wakati huo hakuna mtu anajua  aliko. Alipaswa kuwa amewasili  katika Parokia yake ya Yacoubieh siku hiyohiyo saa za  mchana. Lakini tangu tarehe hiyo hadi sasa hakuna mwenye taarifa yoyote juu yake na pia habari za  abiria wengine waliokuwa naye.

Jitihada za kuwasiliana makundi mbalimbali zinafanywa, ili kama kuna mtu mwenye kujua taarifa zake  atajitokeza. Hata hivyo hisia zimetawala kwamba pengine ametekwa nyara na baadhi ya watu .

Mkuu wa Shirika la Ulinzi katika Nchi Takatifu ametoa wito kwa watu wote , wamkumbuke Padre Dhiya katika sala na maombi yao , na pia kwa waumini wa Parokia yake, Wakristo wa Syria ,  na viongozi wa kiroho na wachungaji na wale wote ambao bado wanaendelea kuyatoa maisha na nguvu zao sadaka katika nchi hiyo, kama mashahidi wa wema kwa watu wote.

Habari zake binafsi zinasema, Padre Dhiya Aziz OFM alizaliwa tarehe 10 Januari 1974, Mosul, Ninawi ya kale, nchini Iraq.  Baada ya masomo ya kuhitimu udaktari wa kutibu watu, bado roho yake haikuridhika , alivutiwa zaidi na maisha ya kumtumikia Mungu kama Mtawa. Na hivyo alijiunga na unovisi huko  Ain Karem, na kuweka nadhiri zake za kwanza tarehe 1 Aprili 2002. Mwaka 2003, alihamishiwa Misri, ambapo alikaa kwa muda wa miaka kadhaa na mwaka 2010 alirudi kutumikia chini ya Shirika  ulinzi katika Nchi Takatifu na kutumwa Amman. Baada ya hapo alihamishiwa Syria, Lattakia. Kisha kwa hiari yake  mwenyewe,alipenda kwenda kusaidia  jamii ya Yacoubieh, katika mkoa wa Orontes (jimbo la Idlib, wilaya ya Jisr al-Chougour), eneo  ambalo limekuwa la hatari  kubwa kwa wasiokuwa waamini wa Kiislamu, hasa   tangu eneo hilo kuwa chini ya udhibiti wa Jaish al-Fatah. Na kwamba , alikuwa ni kati ya waliotekwa  nyara na kundi wanajihadi siku za nyuma , lakini aliweza kutoroka, mwezi Julai 2015.

Taarifa nyingine inasema,  nchini Syria na Iraki wakati wa adhmisho la Sikukuu ya Noel, ghasia za vita na fujo havikusimama, hasa katika eneo ambako kumefanyika mashabulio ya Marekeni yasiyopungua 17 dhidi ya eneo lililotangawa kuwa chini ya serikali ya Kiislamu. Na kwamba, hata Urusi iliendelea na mapambano yake kupitia njia ya anga nchini Syria. Hata hivyo Moscow inasema katika mashambulio hayo hakuna raia wa kawaida aliyedhurika .

Na  Mpatanishi katika juhudi za Kidiplomasia  kwa ajili ya Syria, Stafan De Mistura,ametangaza  uwepo wa duro nyingine ya majadiliano mapya, hapo tarehe 25 Januari mjini Geneva kwa ajili y aupatikanaji amani Syria.  

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.