2015-12-27 15:02:00

Papa Francisko aguswa na maafa Nigeria!


Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa na taarifa ya kulipuka kwa mtambo wa gesi huko Nnewi, nchini Nigeria na kusabisha maafa makubwa kwa watu na mali zao, na wengine wengi kupata majeraha makubwa. Baba Mtakatifu katika salam zake za rambi rambi, zilizoandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu mkuu Augustine Kasujja, anapenda kuwafariji wananchi wote wa Nigeria walioguswa na maafa haya makubwa.

Kwa namna ya pekee, Baba Mtakatifu anapenda kuziweka roho za marehemu wote waliofariki dunia katika ajali hii chini ya huruma ya Mungu; faraja na nguvu kwa wale wote wanaoomboleza kutokana na msiba huu. Baba Mtakatifu anawahakikishia wote uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.