2015-12-26 10:57:00

Baraza la Mawaziri Tanzania limekamilika, Sasa ni kazi tu!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza Baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano ya uongozi wake. Nafasi hizi zinajazwa baada ya tafakari ya kina na ushauri, kutokana na Wizara hizi kuwa na dhamana n anafasi ya pekee katika mchakato wa kuleta mageuzi makubwa katika huduma za kijamii na kiuchumi kwa watanzania wengi!Hapa sasa ni kazi tu!

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.


2. Dkt. Philip Mpango, ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).


3. Mhandisi Gerson Lwenge, ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.


4. Dkt. Joyce Ndalichako, ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)


5. Mheshimiwa Hamad Masauni ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi


6. Prof. Makame Mbarawa, amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano


Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Noeli na Mwaka Mpya 2016 na kuwataka washerehekee kwa amani, utulivu na kiasi. Baada ya sherehe hizi, wakumbuke kurejea kazini kuendeleza gurudumu la maendeleo ya watanzania kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.








All the contents on this site are copyrighted ©.