2015-12-19 14:38:00

Papa akutana na wafanyakazi wa Shirika la Reli Italia


Jumamosi 19 Desemba 2015 Baba Mtakatifu alikutana na wafanyakazi wa Shirika la Reli Italia. Hotuba yake kwa wafanyakazi hao hasa ilikazia maadhimisho ya  Jubilee ya Mwaka Mtakatifu wa kuomba Huruma ya Mungu, aliouzindua hivi karibuni kwamba, zaidi ya yote, unalenga kufundisha na kuweka chapa akilini na mioyoni mwetu  kwamba, huruma ni hitaji la haraka na dawa halisi kwa kila binadamu katika haja zake. Na kwamba huruma kamwe haipungui, bali huendelea kuwepo kwa wingi na kwa mfululizo kutoka kwa Mungu.Na ili tuweze kuipata huruma hi  kutoka kwa Mungu , pia nasi tunapaswa kama hitaji la lazima  kuwa tayari kuwahurumia wengine, ili kila mtu aweze   kuuishi ukamilifu wa ubinadamu wake.

Papa amesema huo ndio ujumbe  tunaokumbushwa wakati wa kupita katika Milango Mtakatifu, inayofunguliwa siku hizi  katika kila jimbo  duniani, kama pia ilivyofanyika katika nyumba ya wageni iliyoko karibu na kituo cha Treni cha  Kati cha Termini Roma,ambako  umefunguliwa Mlango Mtakatifu wa Upendo na huduma isiyokuwa na mipaka katika kusamehe na kufariji,  na katika kutoa msukumo wa kuchangia na kutoa zaidi kwa ukarimu, kwa ajili ya wokovu wa ndugu zetu wahitaji.  Papa aliwaambia wafanyakazi wa Reli wa Italia na kuhimiza wote wajitahidi kufanya upya mapito yao  wanapoelekea katika Mlango huu wa kiroho,  kwa ishara za huduma za kuonekana katika maisha.  Aliendelea kuwaomba, wageuze upya mioyo yao kwa ajili ya  Jubilee ya Huruma ya Mungu , kwa  namna ambamo maisha ya jamii nzima yanaweza kuwa na sura mpya  ya utendaji wa haki zaidi na mshikamano, si nchini Italia tu lakini duniani kote. 








All the contents on this site are copyrighted ©.