2015-12-16 14:24:00

Papa : Maisha ya kila siku na yaandamane na Huruma ya Mungu


Katekesi ya  Baba Mtakatifu Francisco  kwa mahujaji na wageni kwa  Jumatano hii, imelenga katika adhimisho la  Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya kuomba Huruma ya Mungu na pia kukamilika kwa miaka 50 ya uwepo wa  Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican “ dira ya kanisa”.  Papa amehimiza zaidi waamini kuwa na maisha ya fadhila, huruma na msamaha, ishara zinazoonyesha nguvu ya upendo wa Mungu katika kuibadili mioyo migumu  na kufanikisha mapatano na amani duniani.

Papa ameeleza juu ya  ishara za kuonekana zilizofanyika wakati wa Kuzindua Mwaka wa  Jubilee ya Huruma ya Mungu, akisema ishara ya kufunguliwa kwa Mlango Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohana wa Lateran la Roma , Jumapili iliyopita, ilikuwa ni ishara ya kufungua  mlango wa Huruma ya Mungu katika kila Kanisa Kuu la kila jimbo  duniani.  Na  alipenda kusikia kwamba  ishara hii ya  kufunguliwa kwa Mlango Mtakatifu, inafanyika katika kila Kanisa, kwa kuwa  uwepo wa Jubilee ya kuomba Huruma ya Mungu , ni tukio la pamoja na wakati huohuo ikiwa kama ombi binafsi kwa kila mtu. Na kwa namna hiyo  Papa anasema , katika  Mwaka Mtakatifu , Kanisa zima  litatembea katika njia hiyo ya maadhimisho, ambamo  katika kila Jimbo,  kama ilivyokuwa  Jimboni  Roma, Mlango Mtakatifu utafunguliwa kama ishara ya umoja kwa watu  wote.  Papa ameomba umoja  huo wa kikanisa uweze kuwa thabiti  zaidi na zaidi, ili Kanisa liweze kuwa ishara hai ya upendo na Huruma ya Baba duniani.  

Papa aliendelea kueleza pia  kuzinduliwa kwa adhimisho la Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya kuomba  Huruma ya Mungu, akianisha na hitimisho la adhimisho la jubilee ya miaka 50 ya Hati ya  Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Hati ya Kanisa,aliyoitaja kwamba, huwasilisha Kanisa katika mwanga wa fumbo la umoja.  Amesifu hati hiyo iliyoweza  sambaa duniani  kote na kuchukuliwa kama dira na  Makanisa mengi, hasa kama chombo cha kujenga  Kanisa moja tu la  Yesu Kristo, ambamo yeye  mwenyewe aliitoa mafsi yake. Kanisa moja lenye kuishi katika umoja na Mungu.

Papa ameomba,fumbo hili la umoja  wa Kanisa, ambayo ni ishara ya upendo wa Baba, liweze kukua  na kukomaa katika mioyo yetu, kwa utambuzi kwamba,  katika Msalaba wa Kristo, utuwezesha kupendana sisi wenyewe kwa wenyewe kama yeye alivyotupenda. Ni kuwa na upendo usiokuwa na mwisho wala mipaka bali  wenye  sura ya msamaha na huruma.

Papa alieleza na kutoa wito kwamba, huruma na msamaha  isiwe maneno matupu, lakini iwe ni njia ya maisha yetu ya kila siku. Upendo na kusamehe iwe ni ishara wazi na thabiti katika kuruhusu  imani, kubadili mioyo yetu na maisha yetu halisi kwa ajili ya Mungu kama Mungu anavyo tupenda na kutusamehe. Huu ndiyo mpango wa maisha, usiojua usumbufu  au vikwazo katiak kupenda wengine, bali  unatuhimiza kwenda zaidi na zaidi bila kukoma, na tena kwa uhakika  endelevu wa  uwepo wa Baba wa Mungu.

Papa aliendelea kusisitiza juu ya ishara hii ya usharika, kwamba ni ishara kubwa ya maisha ya kikristo, licha ya uwepo wa ishara nyingine nyingi  kama tabia ya Jubilee. Papa ameonyeshamatumaini yake kwamba katika Mwaka huu Mtakatifu wengi wataweza kuvuka moja ya milango Mtakatifu, milango ya kweli ya Huruma ambayo ni  Yesu mwenyewe , aliyesema  “Mimi ni mlango; mwenye kuingia kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka na kupata uzima wa milele "(Yn 10,9).  Papa anasema kuupitia Mlango Mtakatifu ni ishara ya imani yetu kwa Bwana Yesu, aliyesema hakuja  kuhukumu bali kuokoa.  Ni ishara ya mabadiliko ya kweli ya mioyo yetu.  Na wakati wa kuvuka ishara hii ya Mlango Mtakatifu, Papa anasema, ni vizuri kukumbuka kwamba ni lazima pia kuweka wazi mlango wa moyo wetu, katika maana ya  kuwafikia wengine,  na kuwapa habari hii ya upendo wa Kristo. Na kwamba, Mlango Mtakatifu kubaki wazi, ni kwa sababu ni ishara ya kukubalika kwamba,  Mungu ana  nia kwa ajili yetu. Na ndivyo ilivyo,  milango ya mioyo yetu ibaki wazi kwa ajili ya wote bila ubaguzi.

Papa ameeleza na kutaja Ishara  nyingine muhimu katika maadhImisho ya jubilee hii kwamba ni pamoja na  kukiri imani, kupokea sakramenti na hasa kujipatanisha na Mungu , ambao ni uzoefu wa moja kwa moja kwa  huruma yake. Na kwamba hakuna sababu za kuongopa kutubu maana Mungu anaelewa udhaifu wetu  kama binadamu . Lakini ili tuweze kuupata msamaha wa Mungu ni lazima pia sisi tusamehe wengine . Papa anakiri kwamba, ni kweli si rahisi kusamehe , lakini basi tunawezaje kuomba msamaha kwa Mungu iwapo sisi wenywe hatuwezi kusamehe wengine? Ni wazi inakuwa ni ngumu zaidi kusameheh kwa kuwa mioyo yetu ni maskini , na kwa nguvu zetu wenyewe , inakuw asi rahisi kusamehe. Hivyo basi tunapaswa kujifunua wazi katika Huruma ya Mungu kwa ajili yaetu wenyewe na hivyo tunaweza kuwa na uwezo wa kusamehe wengine pia.   Papa alikamilisha na wito wa kuanza kuiishi Jubilee hii na ishara hizi  zenye kutuunganisha pamoja kwa nguvu kubwa ya upendo. Na akamwomba Bwana , kuwa pamoja nasi na kutuongoza katika uzoefu ishara nyingine muhimu katika  maisha yetu.








All the contents on this site are copyrighted ©.