2015-12-10 16:59:00

Wizara ni 18, Mawaziri 19! Hakuna mnuso, fedha kununua madawati!


Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania, Siku ya Alhamisi tarehe 10 Desemba 2015 ametangaza Baraza jipya la Mawaziri kumi na tisa wanaoongoza Wizara kumi na nane. Amefuta matumizi ya shilingi billioni mbili zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya semina elekezi na sasa fedha hii itatumika katika mchakato wa maboresho ya elimu nchini Tanzania. Rais Magufuli amemchagua Dr. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa mambo ya nchi za nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa. Dr. Mahiga kwa aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, Rais Magufuli bado anaendelea kukuna kichwa ili kupata watu wanaofaa zaidi kuongoza Wizara ya fedha na Mipango; Uchukuzi na Mawasiliano; Elimu, sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maliasili na utalii. Wachunguzi wanasema, wizara hizi ni tete zimewahi kuguswa na kashfa za ufisadi na rushwa, kiasi cha kunyooshewa kidole na wadau mbali mbali wa haki, amani na maendeleo ndani na nje ya Tanzania.

Ifuatayo ni hotuba iliyotolewa na Rais Magufuli wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka Ikulu, Dar es Salaam.

Ndugu waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla, ninawasalimu sana. Nawakaribisha katika kikao hiki cha kutangaza Baraza la Mawaziri, Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama.  Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaeelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma ninaiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili.

Wizara ni kama ifuatavyo;

1.Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

Mawaziri - George Simbachawene na Angella Kairuki

Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri - January Makamba

Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri - Jenista Muhagama

MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

 

4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Waziri - Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri - William Ole Nasha

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri : Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

 

6.Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri: Bado hajapatikana.

Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

7.Wizara ya Nishati na Madini

Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.

Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

 

8.Wizara ya Katiba na Sheria,

Waziri - Harrison Mwakyembe

9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri - Dk. Augustino Mahiga

Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

11. Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri - Charles Kitwanga.

12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri - William Lukuvi

Naibu Waziri - Angelina Mabula

 

13. Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri: Bado hajapatikana.

Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

14: Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Waziri: Charles Mwijage.

 

15: Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.

Waziri: Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

16: Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri - Ummy Mwalim

Naibu Waziri – Dkt. Hamis Kigwangala

17: Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo

Waziri - Nape Nnauye

Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

 

18:Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri – Prof. Makame Mbarawa

Naibu Waziri– Inj. Isack Kamwela








All the contents on this site are copyrighted ©.