2015-12-07 16:04:00

Balozi Maria Rivas Elvira wa Perù awasilisha hati zake za utambulisho kwa Papa


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 7 Desemba 2015 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bi Maria Elvira Velàsquez Rivas-Plata, Balozi wa Perù mjini Vatican. Balozi Maria Rivas-Plata alizaliwa kunako mwaka 1956. Ana shahada ya uhusiano wa Kidiplomasia aliyojipatia kunako mwaka 1982 na baadaye akajiendeleza zaidi kuhusiana na matumizi bora ya Bahari na kujipatia shahada kunako mwaka 1987. Kunako mwaka 1985 alianza huduma katika masuala ya kidiplomasia nchini Perù.

Katika maisha yake ya Kidiplomasia amewahi kuwa katibu wa Ubalozi wa Perù nchini Uingereza na mwakilishi wa kudumu wa Perù kwenye Shirika la Mabaharia Kimataifa; Mshauri wa Ubalozi nchini Austria na Mwakilishi wa kudumu wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vienna. Alibahatika pia kuwa ni mwakilishi wa Perù huko Equador na baadaye alikuwa ni Mkurugenzi wa masuala ya bahari na mikataba ya kimataifa. Tangu mwaka 2013 amekua akitoa huduma yake huko MAE kama Balozi wa Perù.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.