2015-12-03 12:23:00

Athari za mabadiliko ya tabianchi kwa Visiwa vilivyoko kwenye Bahari ya Pacific


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 3 Desemba 2015 amekutana na kuzungumza na Bwana Tuilaepa Lupesoliai Sailele Malielegaoi, Waziri mkuu wa Samoa ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu mkuu msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili, wamejikita katika maisha ya kijamii na kiuchumi nchini humo, kwa kupongeza mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi na maendeleo ya wananchi wa Samoa, hususan katika sekta ya elimu. Viongozi hawa wamebalishana mawazo kuhusiana na masuala ya kimataifa; mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi pamoja na matatizo na changamoto zinazojitokeza katika nchi ambazo ziko kwenye Visiwa vya Bahari ya Pacific.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.