2015-12-02 07:49:00

Mkutano wa XIV wa CEP:Idadi ya wasiomjua Kristo yaongezeka


Katika ukumbi wa Mtakatifu Yohana Paulo II, wa  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Jumatatu kulifunguliwa Mkutano wa XIX, wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu (CEP) ulioanza Novemba 30 hadi  Desemba 3, 2015.

Kardinali Giovanni Battista Re, alifungua Mkutano huo kwa Niaba ya Kardinali Fernando Filoni, Rais wa CEP, ambaye  alikosekana kwa kuwa  aliandamana na Baba Mtakatifu Francisco ziarani Afrika.  Hotuba ya  Kardinali Filoni kwa Mkutano huu, ilisomwa na Katibu wa Idara ya Misioni, Mons. Savio Hon Tai –Fai, ambamo ametoa maelezo ya jumla ya  Makanisa machanga, katika eneo la misheni akisema kwa njia ya mikutano ya kawaida,  wamekuwa wakitembea pamoja na Idara ya kazi za Kitume za Missioni, kwa kipindi cha miaka sita. 

Ripoti ya kipindi hicho imegawanyishwa sehemu mbili: kwanza juu ya shughuli za CEP 2009-2015; na  pili ni utendaji w a Makanisa  katika mikoa ya kimissionari kwa  mwanga  wa vipaumbele katika utendaji wake na changamoto wanazokabiliana nazo. Kwa mchanganuo huo, inadhaniwa itasaidia katika majadiliano yao.

Hotuba ya Kardinali Filoni ilirejea takwimu za  Idara ya Propaganda Fide kwamba, idadi ya wale wasiomjua bado Kristo imeongezeka , na kati ya Idadi ya watu wote bilioni saba, Wakatoliki ni bilioni moja .254 ikiwa ni sawa na asilimia 17.7. Na kwamba Idadi ya wabatizwa kwa ujumla iliongezeka katika mikoa ya Misioni, ongezeko kubwa likiwa barani Afrika , ambako mwaka 2005 wakiwa milioni 153 na mwaka 2013 walifikia milioni 206 ikiwa ni ongezeko la asilimia 34 , wakati Marekani kukiwa na ongezeko la asilimia 10.5 na Asia .

Kardinali aliendelea kuzungumzia ukuaji wa  majimbo yaliyokabidhiwa kwa CEP, kutoka  majimbo makuu ya Kikanisa 1,094 kwa mwaka 2009 hadi sasa 1111.  Ili kufanikisha malengo kwa ajili ya jambo hilo, CEP, inashirikiana kwa ukaribu na  Mashirika ya Kipapa  ya Misioni (kama shirika la Uenezaji Imani (Propagada Fidei), Shirika  Mtakatifu Petro Mtume, Shirika la Utoto Mtakatifu, na Shirika la  Umoja  wa  Misioni).  Kardinali amesisitiza umuhimu wa uwepo wa mashirika hayo kwamba kwa kweli  kama mtandao mkubwa katika kimataifa, kitaifa unao fanya kazi kubwa chini ya usimamizi wa Mabaraza ya Maaskofu  majimbo na Parokia. 

Na msimamizi wa Usharika wa kazi za Missioni,  aliainisha shughuli za vyombo vya tegemezi kwa CEP katika huduma,  kwa kutoa maelezo juu ya taasisi zilizo chini ya utume wa Missioni kwamba ni  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana cha Roma, kukiwa na vitivyo vinne na  taasisi shiriki 110 zilizosambaa katika nchi zaidi 40,ambamo jumla ya wanafunzi wapatao 12,000 hushiriki masomo. aliendelea kutaja kwamba , leo hii kaika eneo la Makanisa Machanga kuna jumla ya seminari Kuu 344, kukiwa na jumla ya wanafunzi 26.846 wanaowania Upadre  na kuna seminari ndogo 402 kukiwa na jumla ya wanafunzi 48.727, wakisindikizwa na walezi 2.122.  Hivyo CEP inajukumu la kuhakikisha  upo ufadhili wa kifedha kwa shuel hizo na pia kuandaa wakuu wa taasisi, wakurugenzi wa kiroho , walezi na walimu. Na kwa upande wa imani na mazungumzano kati ya deini , CEP inakazi ya kushawishi uwerpo wa utamaduni wa majdiliano kati ya imani mbalimbali , lakini wakati huohuo kuwa macho na yale yanayoweza kuwa kinyume na imani kwa Kristo kuwa ndiye Mkombozi pekee wa binadamu na ujumbe wa upendo wake. . 

Mwishoni mwa ripoti yake ya kina, Kardinali Filon, alitaja hoja zenye kutia wasiwasi zaidi kwamba ni matumizi mabaya ya utaifa, ukabila na mfumko wa madhehebu mapya yanayoweza ibua migongano na migogoro  hata kati ya waamini wa Kanisa si mijini tu lakini hata vijijini ndani, changamoto inayodai Wachungaji aminifu kufanya kazi kwa bidii  na juhudi za kichungaji, zilizopandwa na wamisionari  wa mwanzo kwa Makanisa machanga. 








All the contents on this site are copyrighted ©.