2015-12-01 15:19:00

Mchango wa Jimbo la Papa kwa Mkutano wa COP21


Jumatatu 30 Novemba, Kardinali Pietro Parolini, alitoa mchango wa Jimbo la Papa, kwa niaba ya Papa Francisko , katika Mkutano wa Viongozi wa Dunia unaotafuta kuweka  makubaliano mapya kwa ajili ya  kusalimisha dunia dhidi ya mabadiliko mabaya ya tabia nchi na hali ya hewa.  Mkutano huo wa  COP-21, uliosubiriwa kwa muda mrefu,  unafanyika Paris Ufaransa, kama hatua inayofuatia kukamilika kwa makubaliano ya Kyoto yaliyomaliza muda wake mwaka huu .

Jimbo la Papa limetoa mchango wake kwa matumani   makubwa kwamba, Mkataba Mpya wa Kimataifa  juu ya  mabadiliko ya tabia nchi , utapitishwa kwa kuzingatia kanuni za umoja na  mshikamano kwa ajili  ya utendaji wa haki, usawa na ushirikiano katika kufanikisha  malengo makuu matatu, ambayo ni kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kupambana na umaskini, na kukukuza  hadhi na ustawi wa binadamu wote, kwa kizazi cha sasa na vijavyo baadaye. .

Hivyo Jimbo la Papa linaomba Makubaliano haya mapya ya kimataifa,   yawezeleta mabadiliko ya  lazima kupitia mihimili  ya nguzo kuu  tatu.  Kwanza ni nguzo inayoshikilia mwelekeo wazi wa kimaadili, katika msukumo wa nia na madhumuni ya utekelezaji wa yatakayoandikwa katika Mkataba, kwa utambuzi kwamba, wanaoishi katika mazingira magumu na wanaopambana na athari za uzushi wa mabadiliko ya tabia nchi,  ni watu  maskini na pia  vizazi vya baadaye ambavyo vinaweza kabiliwa na madhara makubwa zaidi, iwapo binadamu wa sasa hataonyesha kujali matokeo ya utendaji wake kwa sasa kwa siku za  baadaye,  kama wajibu wake.  Hivyo katika utambuzi huo, Jimbo la Papa linahimiza wajibu wa kimaadili  katika kuchukua hatua za utendaji wenye kulinda na  kutetea  mazingira,  kwa mshikamano wa kimataifa, kama wajibu wa kawaida, kulingana na uwezo na masharti yatakayowekwa na wote..

Nguzo ya pili inahusiana na ukweli kwamba,  Mkataba haipaswi tu kuangalia njia za kutekeleza hayo, lakini pia juu ya yote, kusambaza kanuni na ishara wazi  zenye kuongoza mwenendo wa watendaji wote muhimu si tu kwa serikali kuu lakini pia serikali za mitaa, dunia biashara, jamii ya kisayansi na asasi za kiraia. Katika mtazamo huu, nchi zenye rasilimali nyingi zaidi nazenye  uwezo zinapaswa kuongoza na kuwa  mfano,katika haja ya kukuza sera na mipango ya maendeleo na uchumi endelevu.

Nguzo tatu, ni katika mwendelezo wa mazuri yote hata kwa siku za  baadaye, na hivyo  makubaliano haya ya  COP-21, lisiwe tukio la kutia nanga majadiliano hayo lakini ni iwe ni mwanzo wa mchakato huu  muhimu , katika ujenzi wa makubaliano  thabiti zaidi ya pamoja, kupitia taratibu za kuiziishi ahadi  na ufuatilia wake kwa uwazi, ufanisi na nguvu zaidi katika kuchukua  hatua kwa  ajili ya kuongeza kiwango cha hamu ya kuhakikisha udhibiti sahihi wa hali ya hewa  na mabadiliko ya tabia nchi. Pia, ni lazima kufikiria utekelezaji kwa ajili ya uzalishaji endelevu,  matumizi na mitazamo mipya katika maisha ya kijamii.  Na hapo inakuwa ni kuzama katika misingi muhimu ya  ufunguo wa elimu na mafunzo,ambavyo kwa bahati mbaya, wakati mwingine, huishia katika meza za mazungumzo ya mikataba ya kimataifa. Jimbo la Papa limesema, ufumbuzi wa kiufundi ni muhimu, na haitoshi kama haiwezekani  kuingiza  haki ya elimu,  kwa  ajili ya maisha endelevu na uelewa katika uwajibikaji.  Jimbo la Papa limehimiza njia ya maisha ya sasa , pamoja na utamaduni wake wa taka  ambao si  endelevu, ni  lazima kupata  mbadala kwa njia ya elimu na maendeleo endelevu.  Jimbo laPapa limetaja hilo kuwa ni Changamoto kubwa kitamaduni, kiroho na kielimu.

Kardinali alikamilisha maelezo yake kwa kutaja matumaini ya Papa Francisco juu ya mkutano huu  kwamba,  utaweza kukamilika kwa kupitisha Mkataba imara  wa kimataifa,  unaoweza  leta mabadiliko mapya na wazi, katika mwelekeo wa  kimaadili, wenye kuonyesha ishara thabiti kwa wadau wote, kupitisha maono thabiti katika Mkataba wa  muda mrefu, kwa ajili ya ufanikishaji wa malengo matatu , ambayo ni  kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kupambana na umaskini, kudumisha heshima ya binadamu.








All the contents on this site are copyrighted ©.