2015-11-27 14:09:00

Don Mazzucato wa CUAMM afariki dunia


Mkurugenzi wa kihistoria katika Shirika la kujitegemea la  “CUAMM”, Padre  Luigi Mazzucato , alifariki dunia jioni Alhamis 26 Novemba 2015 huko Padova Italia.  CUAMM  ni Shirika linalounganisha Madaktari wa Italia wanaotoa huduma barani Afrika, kwa ajili ya  kuboresha huduma na utetezi wa afya kwa watu maskini barani Afrika. Shirika  hili lililoanzishwa mwaka 1950, huwaunganisha watalaam katika uwanja wa tiba wapatao 1,400, waliotawanyika katika nchi 41 za uendeshaji, wengi wakiwa bara la Afrika,na hasa katika maeneo ya vijijini ambako wanaoishi watu wengi zaidi maskinibila huduma msingi . Shirika hili hufanya kazi zake kwa kushirikiana na Madaktari na Wauguzi mahalia, atika hospitali za wilaya,mashuleni  na katika Vyuo Vikuu vya Tiba.  Afrika Cuamm lina matawi yake Angola, Ethiopia, Msumbiji, Sierra Leone, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.  Aidha Madaktari na wauguzi wanachama wa CUAMM, hufanya kazi zao sambamba na mashirika na taasisi za kimataifa zinazohusika na Madaktari.

 Taarifa kutoka shirika la Cuamm zinassema, Padre Luigi Mazzucato, aliiongoza Cuamm kama Mkurugenzi wake Mkuu tangu mwaka 1955 hadi 2008,  kwa ujasiri mkubwa wa akili, na uwezo wa ajabu katika upatanishi wa kinabii, aliweza ongoza shirika kwa ujasiri na kama kiongozi  imara, na hasa kama  mwalimu wa maisha kwa watu wengi waliomfahamu. Kipindi chote  alichochukua  changamoto ya kuongoza Cuamm,  alifanya kazi kwa  moyo wa kujitolea na kujituma bila kujibakiza , akiwa na tabia ya kutafuta  yaliyo mema zaidi kuliko hila na shutuma.

 Don Dante Carraro, Mkurugenzi wa sasa wa Cuamm Afrika, amesema, Marehemu Padre Luigi ataendelea kukumbukwa kwa mengi na hasa kwa jina la utani la  upinde wa mvua, katika kuwahudumia  maskini,  aliowataja kuwa urithi wa Mungu; watu aliowapenda siku zote akitafuta kuwajua zaidi na zadi , kuwasikiliza na aliiweka mipango yote ya CUAMM katika kudra mpango na uaminifu wa Mungu kwa  nyakati zote, katika  sala na matumaini mapya yaliyolisha daima maisha yake.

Na kwamba , katika maisha yake  ya kuiongoza Cuamm, pia alikumbana na changamoto  nyingi  na ngumu, katika safari zake zaidi ya mia alizozifanya Afrika, ambako alijionea hali halisi za umaskini wa watu.  Na kwa  uchungu, mwaka 1987, alifungua hospitali ya kwanza ya vitanda 40 kwa ajili ya kulaza  wagonjwa wa UKIMWI,  katika eneo la Aber nchini Uganda, ambako watu walikuwa wakimalizwa vibaya na ukimwi.  Aidha aliguswa vikali na wahanga wa maasi nchini Msumbiji, na mauaji ya kimbari nchini Rwanda (1994), hali ya utapiamlo mkali kwa watoto nchini Ethiopia. Pia mateso ya umasikini Guinea Bissau, na Angola uliosababishwa na migogoro ya ndani, na hivi karibuni, umaskini uliokithiri nchini Sudan Kusini.

Padre Dante anaendelea kurejea ukarimu wa Marehemu Padre Luigi ambaye katika hotuba yake tarehe 11 Novemba 2010, wakati wa sherehe za kupewa shahada ya heshima kwa utetezi wa  haki za binadamu na amani, iliyotolewa na  Chuo Kikuu cha Padua , alisisitiza kwamba maisha yake yaliongozwa na kanuni za Cuamm. Na kwamba utume wa Injili, ndiyo madhumuni ya Cuamm. Pia alisisitiza Uhuru katika uchaguzi wa hatua za kuchukuliwa ili kufikia malengo ya kazi yao: huduma kwa wagonjwa na , maskini katika  nchi maskini, na hasa wale wanaonyimwa uhuru wao na kulazimika kuishi katika mazingira magumu na  hatarishi. 

 Don Luigi Mazzucato alizaliwa Saccolongo Padua Italia,  Januari 8, 1927. Alipadrishwa mwaka 1950. Mwaka 1955 alipata shahada yake katika theolojia katika Chuo Kikuu Gregorian cha Roma.   Na katika maisha ya Don Luigi Mazzucato akiiongoza Cuamm, aliwafadhili wanafunzi 280 kutoka nchi maskini 32 na pia mamia kadhaa ya wanafunzi kutoka Italia. 








All the contents on this site are copyrighted ©.