2015-11-25 13:46:00

Siku ya Kimataifa ya kufuta maonevu kwa wanawake


Kila mwaka tarehe 25 Novemba, ni  Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza unyanyasaji na  Ukatili kwa Wanawake. Siku hii iliwekwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutetea  Haki za wanawake zinazokwenda sambamba na haki za  Binadamu. Na hivyo ni kampenni kwa ajili ya kuleta mwamko zaidi katika kukomesha unyanyasaji wa Kijinsia. Kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana duniani kote .

Kihistoria, msingi wa tarehe hii  inatokana na mauaji ya mwaka  1960 ya wanawake watatu ,  wanaharakati wa kisiasa katika Jamhuri ya Dominika, waliouawa kwa amri ya Dikteta wa Kisiwa cha  Dominika , Rafael Trujillo, mauaji yaliyoitaja Novemba 25,  kama siku ya kupambana na kuongeza uelewa  juu ya madhara ya unyanyasaji na ukatili  kwa wanawake kwa mapana zaidi. Siku hiyo ilipitishwa na Umoja wa Mataifa Desemba 17, 1999, kama azimio la Umoja wa Mataifa.  

Kwa azimio hiyo , kila mwaka 25 Novemba, Umoja wa Mataifa hutoa wito kwa Serikali, Mabunge ,  mashirika ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuandaa shughuli za kusaidia  kuleta mwamko zaidi kwa ajili ya Siku hii ya kimataifa.  Kwa mfano,  kutangaza kwa bidii zaidi,  Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake. Pia kutoa  mapendekezo kwa mashirika mengine, kujihusisha zaidi na utetezi wa haki za wanawake  kama jambo la lazima.. mfano kwa mwaka 2014, lengo lilikuwa ni kwa jinsi gani inawezekana kupunguza vurugu  za majumbani na maeneo mengine  kama ilivyoainishwa katika  Azimio la Beijing na Jukwaa la Utendaji  katika kipidi cha miaka 20 ijayo.

Azimio lilitokana na Mkutano wa  Beijing wa mwaka  1995, miaka  20 iliyopita, lilizishirikisha serikali 189, katika mkutano wa  Wanawake wa  mjini Beijing, kama tamko la Utendaji ,ilikariri mikakati muhimu ya kukomesha ukatili kwa wanawake, kuwawezesha wanawake, na kufikia usawa wa kijinsia. Umoja wa Mataifa unasema, ahadi hiyo ya miaka 20 iliyopita bado ni halali hata leo.  Na sasa ni wakati wa kuchukua hatua.

Kwa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , ametoa wito kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kujiunga katika kampeni hii, iliyoitwa “ tuungane” “Dunia ya rangi ya chungwa”, kampeni  itakayoendelea hadi Desemba 10, 2015.

Azimio hili la Beijing linasema, unyanyasaji dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki za binadamu.  Na kwamba , ukatili dhidi ya wanawake ni matokeo ya ubaguzi kwa wanawake katika mifumo mingi ya maisha  na ya kung'ang'ania mila zinazotoa hadhi tpfauti kati ya wanaume na wanawake, senye kutaka kugandamiza wanawake.Lakini elimu ya sayasi ya watu inasema, unyanyasaji dhidi ya wanawake  huathiri maendeleo katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na juhudi za kupambana na  umaskini, maradhi kama VVU / UKIMWI, na uwepo wa amani na usalama katika jamii.

Na kwamba, unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana ni jambo linalozuilika au kuepukwa  na ni muhimu kuwa hivyo,  vinginevyo litaendelea kuwa  janga la kimataifa lenye kurudisha nyuma ustarabu na maendeleo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa , asilimia 35% ya wanawake na wasichana duniani , huishi katika hali mbalimbali za maonevu, vurugu na madhulumu hasa katika mahusiano ya mapenzi na mgono katika maisha yao. Na kwamba katika kila kundi la wanawake kumi,kati yao  hadi saba hukabiliwa na unyanyasaji huu katika baadhi ya nchi. Na kwamba duniani kote, wanawake zaidi ya milioni 700, wameolewa wakiwa na umri mdogo, kama  watoto kati yao  milioni 250 kabla ya  umri wa miaka 15. Jambo linaloathiri kwa kiwango kikubwa, nafasi  ya kukamilisha masomo au uwezo wao wa kujiendeleza kimasomo .  








All the contents on this site are copyrighted ©.