2015-11-24 16:51:00

Dr. Gian Franco Mammi ateuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne, tarehe 24 Novemba 2015 ametembelea kwenye Benki ya Vatican, IOR ili kujionea shughuli zinazotendwa kwenye taasisi hii ya fedha ya Vatican ambayo imefanyiwa marekebisho makubwa ili iweze kutekeleza dhamana na wajibu wake katika ukweli na uwazi, tayari kusaidia mchakato wa shughuli za Uinjilishaji zinazofanywa na Mama Kanisa sehemu mbali mbali za dunia.

Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anafafanua kwamba, Baba Mtakatifu amepata pia nafasi ya kukutana na kuzungumza na Bodi ya wakurugezi wa Benki ya Vatican. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Dr. Gian Franco Mammi kuwa Mkurenzi mkuu wa Benki ya Vatican. Kabla ya uteuzi huu, Dr. Gian Franco Mammi alikuwa na Kaimu mkurugenzi wa Benki ya Vatican. Nafasi ya Kaimu mkurugenzi wa Benki ya Vatican itasimamiwa kwa sasa na Dr. Giulio Mattietti, wakati wakisubiri uteuzi rasmi wa Kaimu mpya wa Benki ya Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.