2015-11-14 07:19:00

Balozi Claude Joel Giordan awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 13 Novemba 2015 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Claude Joel Giordan wa Ufalme wa Monaco aliyezaliwa kunako tarehe 27 Desemba 1949 huko Monaco. Ameoa na amebahatika kupata watoto wawili. Balozi Giordan ni mtaalam wa masuala ya sheria na sayansi za kisiasa na utawala bora. Ni kiongozi mwenye ujuzi na kwamba, tangu kunako mwaka 1975 amekuwa katika utumishi wa umma kwa nafasi mbali mbali.

Amekwisha wahi kuwa Mkurugenzi mkuu wa kazi na maendeleo ya kijamii kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1977. Kati ya mwaka 1978 hadi mwaka 1982 aliteuliwa kuwa mkurugenzi msaidizi katika idara ya fedha na uchumi. Kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1990 alikuwa ni mkuu wa idara ya fedha na uchumi kazi aliyoitekeleza hadi kunako mwaka 1995. Kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 2001 aliteuliwa kuwa mshauri mkuu katika Ubalozi wa Ufaransa na kati ya mwaka 2001 hadi mwaka 2004 aliteuliwa kuwa Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Kunako mwaka 2005 aliteuliwa kuwa balozi nchini Ujerumani na katika mashirika ya kimataifa ya OSCE, AEIA na Balozi asiye mkazi nchini Austria, Poland na Russia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.