2015-11-09 13:49:00

Baraza la Kipapa lawatakia Wahindu wote Sikukuu njema ya Diwali


Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo  kati ya dini , limepeleka salaam za matashi mema na ujumbe wake kwa ajili ya Sikukuu ya Diwali, ambayo huadhimishwa na wafuasi wa dini ya Kihindu duniani koke, mwaka huu ikiwa Jumatano, tarehe ll Novemba 2015.  Baraza la Kipapa limetoa ujumbe wake kwa matumaini kwamba, Sikukuu hii, itaweza kuwa kichocheo au chemichemi ya furaha na amani ya kudumu katika familia za wahindu na jamii yao na dunia kwa ujumla.

Salaam hizo zilizotiwa saini na Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya mazungumzo na dini nyingine Kardinali Jean Louis Tauran  na Katibu wa Baraza hilo zimerejea waraka wa  Baba Mtakatifu Francisco  wa Laudato Si,ambamo mnamzungumzia uhusiano wa  binadamu  na migogoro inayokabili mazingira katika  dunia yetu kwa nyakati hizi zetu.  Baraza linasema, kwa hiyo,  inakuwa ni jambo jema, kushirikishana baadhi ya mawazo, katika haja ya kukuza viungo vipya katika  muungano wa ekolojia ya binadamu.  Ekolojia ya binadamu yenye kuwa na uhusiano na wajibu  katika kutunza fadhila za mazingira ya dunia. Baraza limetaja miongoni mwake ikiwa ni matumizi kadhaa ya  rasilimali endelevu ya ardhi kwa njia ya kupitishwa kwa sera; kitaifa na kimataifa, zenye kuheshimu  viungo vinavyotegemeana  kati ya binadamu na viumbe na  maumbile, kama hoja muhimu,  ​​kwa ajili ya afya ya dunia yetu, ambayo ni nyumba ya familia ya binadamu,si kwa nyakati hizi tu  lakini pia kwa vizazi vijavyo.

Ujumbe unaendelea , bahati mbaya,baadhi ya watu binafsi au makundi ,  ubinafsi wao huonyesha dhahiri  katika matumizi  na tabia mbaya za ulafi wa mali  na kutojali mazingira, ubinafisi wenye kulishwa  na hamu ya kutenda kama ni "mabwana" watawala , badala ya  kuwa “walezi" na "walinzi" wa asili.  Aidha umesisitiza kuwa, binadamu wote wana jukumu bila kujali imani za kidini au utambulisho wa taifa, kuishi na wajibu mkubwa wa kuilinda asili, na kuendelea kutengeneza  mahusiano muhimu chanya na zaidi ya yote, kujipanga vizuri vyema katika njia  ya maisha na miundo ya kiuchumi kulingana na changamoto ya kimazingira zinazo tukabili kwa wakati huu.  Na kwa kufuata  mafundisho ya dini yao ya Kihindu, husisitiza  mshikamo wa umoja wa asili, ubinadamu na Mungu. Na  Imani ya Kikristo hufundisha kwamba, dunia iliumbwa na kukabidhiwa kwa binadamu na Mungu mwenyewe kama  zawadi  kwa binadamu wote. Na hivyo binadamu anakuwa na wajibu wa kuilinda na kuiheshimu  dunia na kuihudumia  kwa uwajibikaji thabiti katika utoaji wa maamuzi juu ya  matumizi ya viumbe vya dunia.

Aidha salaam hizo zimekumbusha  uwepo wa  uhusiano katika mambo yanayowaunganisha binadamu moja wapo ikiwa ni amani kwa watu wote.  Amani inapaswa kutawala  dunia,  hii ikiwa na maana ni haki ya kila mtu, iwe binafsi au kama kundi,zikiwemo huduma kwa mambo asili, kama ilivyoelezwa katika kipengere cha utetezi wa maskini  na ujenzi wa mtandao wa heshima na udugu na Papa Francisko katika waraka wa Laudato Si. Na kwamba, uendelezaji wa mazingira ya binadamu unahitaji mafunzo na elimu katika ngazi zote, kwa ajili ya ufahamu na wajibu wa mazingira na ulinzi wa busara, kwa  rasilimali ya dunia, kuanzia na familia,  kama msingi  na muundo wa ''ekolojia  ya binadamu, ambamo ndani mwake mtu hupewa mawazo yake ya kwanza ya ukuaji kuhusu ukweli na wema, na kujifunza nini maana ya upendo na kupendwa, na hivyo nini  maana ya kuwa mtu "(Yohane Paulo II, Centesimus Annus, 39). Kwa hiyo , ni juu ya miundo ya elimu na jukumu la serikali kutoa mafunzo  kwa wananchi na ufahamu sahihi  juu ya  viumbe na mazingira ya binadamu na uhusiano wake binadamu na viumbe.

Na hivyo kwa  ubinadamu wetu na uwajibikaji  wa pamoja, kimaadili na kiimani, Wahindu na Wakristo, pamoja na watu wa mila nyingine za kidini na wote wenye mapenzi mema, wanaweza  kuboresha utamaduni wa ubinadamu katika kutunza mazingira. Na hivyo kwa njia hiyo  kutakuwa na maelewano ya kina kati ya binadamu na katika uhusiano viumbe vingine, na asili yote iliyoumbwa na Mungu, na hili "linakuwa ni chemichemi ya  neema  ya ukuaji wa 'mti wa amani"kama ilivyoelezwa na Papa Mstaafu Benedikto wa XVI. 
 








All the contents on this site are copyrighted ©.