2015-11-06 14:54:00

Mchango wa Kanisa katika kukabiliana na changamoto za elimu kwa vijana!


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 6 Novemba 2015 amekutana na kuzungumza na Gavana Cècile Ellen Fleurette wa Grenade, ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na mgeni wake Gavana Cècil, wameshukuru na kupongeza mahusiano mema yaliyopo kati ya Vatican na Grenade pamoja na mchango wa Kanisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wa Grenade, hususan katika kukabiliana na changamoto za elimu miongoni mwa vijana wa kizazi kipya. Mwishoni, wamejadili pia masuala ya kimataifa na kikanda katika eneo la Caraibi, kwa kujikita katika matatizo na changamoto za kiuchumi, uharibifu wa mazingira, nyumba ya wote pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watu na mali zao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.