2015-11-02 14:44:00

Papa asema Watakatifu si tu waliotangazwa na Mama Kanisa lakini pia wapo tunaoishi nao kila siku


Baba Mtakatifu Francisko Jumapili akihubiri katika Ibada kwa ajili ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Watakatifu wote, alilenga zaidi katika somo la Injili, ambamo mna mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake juu ya Heri, aliyoyatoa katika  kilima,  karibu Ziwa la Galilaya.

Papa alisema, Neno la Bwana Mfufuka na Hai,  pia hata kwetu leo hii , linatuonyesha sisi kwamba, kujiunga katika  njia ya maisha ya  heri, ni njia inayo tuongoza kufika mbinguni. Papa aliongeza pengine inaweza onekana kuwa njia ngumu katika kuifuta., kutokana na ukweli kwamba, inatuhimiza kwenda kinyume na pepo za mambo ya kidunia. Lakini  Bwana anatuambia kwamba wale wanaotembea katika barabara hii ya kuishi kwa heri, huwaongoza katika kupata furaha kamili, iwe  kwa maisha ya sasa au ya baadaye, kwa kuwa hupokea yote katika maisha yao huzuni. mateso na  furaha kama sehemu ya maisha. 

Papa alizingumzia heri hizo, "Heri walio maskini wa roho , maana wataurithi ufalme wa Mungu , akisema ni kwa namna gani mtu anaweza kuwa na furaha iwapo roho yake ni maskini? Na kufafanua kwamba, watu hao huwa na furaha kwa kuwa mioyo yao ni huru dhidi ya wasiwasi na mambo ya kidunia. Ni watu wanaojali huzuni na maumivu ya wengine, wakiwa wamejawa na furaha ya kupokewa katika Ufalme wa Mbinguni ambako wataweza kuiishi huruma ya Mungu na faraja  zake katika Maisha yao wenyewe. Papa alieleza na kuongeza hawa watakuw ana furaha  kwa sabab u watakuw akatika Mkono wa Mungu , Baba wa faraja zote.

Adiha Papa alieleza juu ya Heri walio wa Wapole ambao wako kinyume na wengi wasiokuwa na uvumilivu, wenye wasiwasi na ambao wako tayari kulalmika kwa kila linalofanywa na wengine. Watu walalamishi. wenye kujiona kama peke yao ndiyo mabwana wa dunia, n akumbe sote tu wana wa Mungu.  Papa alieleza na kutoa mfano wa wazazi ambao daima huwavumilia watoto wao. Alisema kuwa hiyo ndiyo ndiyo ya kutembea na Bwana . Ni njia ya upole na unyenyekevu iliyofuatwea na Yesu  , tangvu akiwa mtoto hadi kipindi cha kuteswa na kushitakiwa mahakamani , yote aliyapokea kwa nyenyekevu mkubwa hadi kifo chake msalabani kwa ajili ya wokovu wetu.  Na hapo ndipo kuna mzizi wa wito wa utakatifu. Na kwamba katika adhimisho hili la Siku Kuu ya Watakatifu wote, tunawakumbuka wote walioishi neema hiyo ya Ubatizo, ambao waliweza kuitunza kama alama na kutembea nayo kama wana wa Mungu , wakitafuta kumwiga Kristo , na sasa wameungana naye , na wanamwona Mungu alivyokuwa na hata sasa.

Papa alieleza na kusisitiza zaidi umuhimu wa kuyaiga maisha ya Watakatifu akisema , si tu kwa wale waliotajwa kuwa Watakatifu lakini pia hata kwa wale wanaoishi karibu yetu , ambao wamejaliwa neema hii na Mungu , kuiishi Injili kwa namna ya kipekee katika maisha yao. Hao ni Watakatifu tunaokutana nao pia sisi katika maisha yetu ya kila siku, na pengine tunaishi nao ndani ya  familia zetu au kati ya wafanyakazi wenzetu au kati ya marafiki  na watu wengine tunao wafahamu.

Papa alieleza na kutaja umuhimu kumshukuru Mungu kwa ajili ya uwepo wao, kama zawadi aliyoiweka karibu na sisi , wakiwa mfano hai , unaoweza kutuambukiza katika jinsi ya kuishi na hata kufariki na imani kwa Bwana Yesu, na Injili yake.  

Na "heri walio na huruma, maana watahurumiwa. Papa amewataja kuwa ni watu wenye kufurahi kwa kuwa wanatambua kuwa nao watasamehewa . Ni watu wanaopenda kusamehe na si kuhukumu wengine. Wanapenda kujiweka katikaviatu wengine. Papa alieleza na kuasa kwamba Msamaha unapaswa kutolewa bila ubaguzi.  Na si kama ni lazima iwe kwa hotuba rasmi lakini ni utendaji wa kawaida katika kuwa  wakweli. Ni kusema "Bwana, mimi hapa, nihurumie." Na  kwa jinsi sisi tunavyopenda tusamehewe pia sisi tuwe wepesi wa kusamehe wengine kama tunavyo sali kila siku siku katika sala ya "Baba yetu": "Utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wanao tukosea.








All the contents on this site are copyrighted ©.