Juhudi zote za Mkristo katika imani ni kwa ajili ya kumkaribisha Roho Mtakatifu moyoni. Ni ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisco wakati wa Ibada ya Misa katika Kanisa ndogo la Mtakatifu Marta hapa Vatican. Papa alisisitiza kwamba, wogofu wa moyo kwa Mkristo , ni utendaji wa kila siku unaoongoza katika njia ya kukutana na Yesu .
Na hivyo kwa Mkristo wogofu ni wajibu. Ni jukumu analopaswa kulifanyia kazi kila siku . Papa alileleza hilo kwa kurejea somo kutoka Kitabu cha Mtakatifu Paulo kwa Warumi ambamo amesisitiza kwamba ili kuondokana na maisha ya dhambi hadi maisha safi Matakatifu ni lazima kuwa na bidii za kufanya hivyo kila siku.
Papa alieleza kwa kurejea Mfano uliotumiwa na Mtakatifu Paulo, mfano wa mwanamichezo,
kwamba hujiandaa mwenyeweili apate ushindi mkubwa. Na ndivyo hata Mkristo anavyotakiwa
kujiandaa kila siku kwa ajili ya kuwa mshindi dhidi ya dhambi. Mtakatifu Paulo, Papa
alisema "anatuhimiza kusonga mbele na juhudi hizi.
Papa alihoji iwapo huwa tunafikiri kwamba utakatifu huja kupitia juhudi tunazojifanya
wenyewe, kama ilivyo kwa mwanariadha anayetafuta ushindi kwa njia ya mafunzo? Ni kweli
kwamba juhudi zetu tunazojifanya, katika kazi zetu za kila siku katika kumtumikia
Bwana kwa moyo wote, na akili yote na mwili wote , pamoja na maisha yetu yote, hufungua
mlango kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huweza ingia ndani mwetu na kutukomboa!
Yeye ni zawadi ya Yesu Kristo! Vinginevyo, utendaji wetu unakuwa bure. Juhudi zetu
ndizo huweza fungua mlango kwa Roho Mtakatifu.
Baba Mtakatifu alieleza huku akionyesha kutambua kwa jinsi ilivyo vigumu , kutokana
na udhaifu wetu , unaotokana na uwepo wa dhambi ya asili yaani shetani, ambaye daima,
hutuweka katika majaribu ya kuturudisha nyuma, kama waraka kwa Waebrania , unavyo
onya dhidi ya majaribu ya kugeuka nyuma. Unaonya tusirudi nyuma, au kuanguka tena
katika dhambi, lakini ni kusonga mbele katika hatua za utakatifu siku hadi siku, hata
wakati wa shida na matatizo makubwa. Papa alieleza na kuhimiza waamini wa Kristo
kutafuta neema za Mungu kwa bidii zote, kama ilivyo kwa mwanamichezo anayepania kupata
ushindi mkubwa katika michezo, hujibidisha katika mafunzo.
Na alionya kwamba baadhi majaribu ni tamaa za uzushi mambo kwa wengine. Kuishinda tamaa hiyo Papa anasema ni kufanya jitihada za kukaa kimya. Vinginevyo, hatuwezi kuyashinda majaribu, na hivyo tunakuwa dhaifu na kupoteza bidii ya kusali. Lakini pia Papa alisema, mara nyingi ndani mwetu hata tunapo poteza bidii, hubaki mbegu ndogo ya kufanya hivyo. Mbegu hiyo ndogo hutusaidia kutoanguka moja kwa moja chini, au kurudi nyuma kabisa katika uovu. Lakini huTUsaidia kusonga mbele katika kuielekea zawadi hii, ambayo ni ahadi ya Yesu Kristo, katika haki ya kukutana naye. Papa alirudia tena , kutoa mwaliko wa kuomba neema hii ya kukutana na Bwana. Kuwa na nguvu, kuwa imara katika mafunzo haya kuelekea kukutana na Bwana wa maisha, hadi kuipokea ile zawadi ya kuhesabiwa haki, zawadi ya neema, zawadi ya Roho katika Kristo Yesu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |