2015-10-21 16:38:00

Muhtasari wa vikao vya Sinodi kwa Jumatano 21 Oktoba


Katika Mkutano wa Jumatano kwa ajili ya kutoa taarifa fupi kwa wanahabari, wageni waalikwa waliofika katika mkutano huu tokea Ukumbi wa Sinodi ya Maaskofu ni  Kardinali Marx, ambaye ni Askofu Mkuu wa Munich-Freising na Rais wa Baraza la Maaskofu  Ujerumani na  sauti ya mamlaka ya Ujerumani, katika majadiliano ya kidunia; pia alikuwa ni Kardinali Berhouet Sturla, ambaye ni askofu mkuu wa Montevideo, Uruguay, na mwakilishi wa Amerika ya Kusini; na  Askofu Mkuu  Eamon Martin, Askofu Mkuu wa Armagh, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki  Ireland,  pia alikuwa katibu wa moja ya kundi dogo kwa ajili ya kupaa mtazamo kwa makundi yanayozungumza Kiingereza.


Padre Lombardi, alionyesha matumaini yake kwamba, wanahabari hao tayari walikuwa wamesoma taarifa za makundi 13, walizopewa mapema asubuhi na Ofisi ya uchapishaji ya Vatican, kama zilivyosoma Jumanne jioni na wawakilishi wa vikundi vidogovidogo kwa Sekretarit ya Sinodi , kwa ajili ya kazi ya kuunganisha taarifa hizo.Na kwamba kulikuwa na michango zaidi ya 500 na hivyo ilikuwa ni kazi kubwa katika sehemu hii ya tatu.  

Hata hivyo , Msemaji wa Vatican, kabla  ya kuwakaribisha wageni waalikwa rasmi kutoa kwa wanahabari waliyokuwa nayo, alipenda kwanza kutoa neno kwa habari zilitolewa usiku wa kuamkia Jumatano, habari za uzushi juu ya afya ya Papa. Hivyo alichukua nafasi hii, kuthibitisha kwa wanahabari kwamba, yote yaliyoelezwa ni uzushi. Na alisema hivyo baada ya kuwasiliana na vyanzo sahihi juu ya afya ya Papa, ikiwa ni pamoja na Papa mwenyewe.

Na kwamba, hakuna daktari wa Kijapan aliyekuja  Vatican kuonana na  Papa; na wala hapajafanyika vipimo vyovyote vya aina hiyo na wala hakuna helkoputa yoyote iliyowasili Vatican kutoka nje , hata kwa mwezi Januari kwa ajili hiyo, hivyo yaliyo andikwa ni habari ya uongo.

Padre Federico Lombardi alirudia kusema kwa kifupi taarifa iliyotolewa ni uzushi . Na akasema anathibitisha kwamba Papa ana  afya njema ...  kama alivyoonekana wakati wa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kipindi cha asubuhi. . Na kama wote wanavyofahamu ana tatizo la  mguu, na si kichwa.

Na kwamba uchunguzi mdogo uliofanywa kwa Gazeti lililochapisha habari hiyo  juu ya Papa, mapema Jumatano, karibu yake  kulichapishwa mahojiano ya ujumla na mwanahabari kwa Prof.  Maira, kuhusu uvimbe wa ubongo. Prof. Maira akizungumza tokea New York,  kwa njia ya simu, alionyesha kushangazwa na kilichoandika akisema, yeye hajui chochote juu ya habari hii ya Papa . Na kwamba wakati wa mahojiano aliyofanya na  Mwandishi wa habari juu ya maradhi ya kansa ya ubongo, alitoa maelezo ya jumla, na hakusema lolote linalohusiana na habari iliyo chapishwa. Na hivyo amepokea habari iliyotolewa kwa mshangao  mkubwa pia ..

Papa Federico Lombardi alieleza hilo na kukemea kwamba  uchapishaji wa taarifa kama hii ni kitendo cha kukosa uwajibikaji, na mhusika hana namna ya kujitetea bali kuwajibishwa. Na pia haifai kuendelea kuandika au kudadisi zaidi juu ya uzushi huu usiokuwa na msingi. Na hivyo aliufunga mjadala huo mara moja.
 








All the contents on this site are copyrighted ©.