2015-10-21 15:17:00

Msemaji wa Vatican asema, Papa ana afya njema


Mkurugenzi wa Ofisi ya habari ya Vatican, Padre Federico Lombardi, akizungumzia afya ya Baba Mtakatifu Francisko anasema yu mzima, na anaendelea na kazi zake za kila siku. Padre Lombardi ameeleza hili, kufuatia habari za uongo zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari juu ya afya ya Baba Mtakatifu Francisko.

Padre Lombardi amerudia kueleza hili baada ya kupata taarifa za kweli kuhusu afya ya Papa Francisko kutoka kwa wanaohusika na afya ya Papa . Na kwamba hakuna daktari  wa Kijapan aliyemtembelea Papa hivi karibuni Vatican na na wala hapajawa na aina yoyote ya vipimo alivyofanya Papa kama inavyodaiwa katika habari iliyoandikwa. Na ofisi husika za Vatican zimethibitisha kwamba hakuna madaktari wowote waliowasili Vatican kwa njia ya helkopta, kutoa huduma kwa Papa  na wala hapajawa na wageni wa aina hiyo mwezi Januari.

 Msemaji wa Vatican, ameeleza na kusema Papa ana afya nzuri. Na akaonya kwamba uchapishaji wa habari kama hizi za uongo ni kosa kubwa na ni  kitendo cha kukosa uwajibikaji, na hakuna namna, mwandishi huyo anavyoweza kujitetea au kutowajibishwa.  Hivyo Padre Lombardi aliwataka waandishi wa habari kutoweka mafuta katika habari za namna hii za uzushi na uongo usiokuwa na msingi. Na hivyo akawaambia wanahabri kwamba suala hili halina mjadala, na analifunga mara moja. 








All the contents on this site are copyrighted ©.