2015-10-20 14:47:00

Papa :Upendo wa Mungu usio na ukomo, huwaendea wote wanaoridhia


Upendo wa Mungu usiokuwa na kipimo huwandea watu wote wanaomtafuta na kumwamini. Upendo wa Mungu, daima ni tunda la neema zake ambazo huzitoa kwa watu wote.Na kwamba Mungu daima yu tayari kusamehe na kuwapokea wanaotafuta kumrudia na huwa na subiri kama Baba anavyomsubiri mtoto wake aliyepotea. Maneno hayo yamekuwa kiini cha  homilia ya Papa Francisco, wakati wa Ibada ya Misa ya  asubuhi, aliyoadhimisha katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta.

Baba Mtakatifu alitafakari upendo wa Mungu usio na kipimo  kwa watu wote.  Ukarimu na huruma ya Mungu inayo puuzwa na kuepukwa na binadamu, katika mazoea ya kujiamulia kama anavyotaka kama vile hakuna Mungu. Papa Francisco alieleza kwa kurejea kifungu maneno ya Mtume Paulo, ambamo amesisitiza kwamba, Ukombozi uliletwa na Yesu, baada ya Adamu kuanguka katika dhambi. Wokovu huu wa Yesu ni tendo kuu lililojenga urafiki kati yetu na Mungu.

Papa aliendelea kueleza kwamba, wakati ulipotimia kwa mapenzi yake, Mungu alijenga urafiki na wokovu kwa watu wote. Wakati ulipotimia alitupa nafasi sote ya kukomblewa na upendo wake usiokuwa na mwisho, upendo uliojaa wingi wa neema kwa wale wanaomkubali na kumpokea katika mioyo yao . Papa aliendelea kuzungumzia neno hili la wingi , ambalo katika kifungu hiki cha maneno ya somo lililosomwa yamerudiwa kwa mara tatu, akisema, Mungu anatoa kwa wingi tena kwa uhakika kama Mtume Paulo alivyoeleza mwishoni, mahali palipo na dhambi pamejaa neema,  Pamefurikwa na neema, na huo ndio upendo wa Mungu usiokuwa na kipimo. Na kwamba ni Mungu mwenyewe anayetoka na kwenda nje, kama ilivyoelezwa katika mfano wa  somo la Injili,ni kama  baba mwenye kusubiri kwa hamu, akitazama upeo wa nchi kuona kama mtoto wake aliyeondoka ameamua kurudi nyumbani. Vivyo hivyo Papa anasema, Mungu haufungii upendo wake lakini  daima ni wazi kwa wote wanaomtafuta. Na mara wanaporejea hupokelewa kwa shangwe na kwa  upendo mkuu , akiwakumbatia kama watoto wake, kufanya Sikukuu.

Papa aliendelea kueleza Mungu si Mungu bahili, na wala hajui udhaifu, lakini hutoa kila kitu kwa kil anaye mwendea. Na kwamba utendaji wa Mungu hausimama, lakini huendelea siku sote kuonekana, na hutusubiri tubadilike.  Mungu ni Mungu mwenye kutoka nje kwenda kutafuta, humwangalia kila mmoja wetu. Kila siku yeye yupo kwa ajili yetu, hivyo ni sisi tu tunaotakiwa kubadilika na kuyaweka maisha yetu yote kwake, Naye atatenda yote katika maisha yetu. Yeye hufanya kama alivyosema, nitawatafuta wanakondoo wangu waliopotea,  pia kama unavyosema mfano wa sarafu moja ikipotea kati ya tisini na tisa .

Papa aliendelea kuzungumzia furaha ya Mungu kwa mmoja wa wadhambi anapoongoka na kuwa mtu mwema. Na kwamba Mungu anatambua si rahisi, katika viwango vyetu kibinadamu, kuelewa upendo huu wa Mungu hata chembe yake ndogo. Lakini kwa neema zake tunaweza elewa.

Baba Mtakatifu alihitimisha homilia yake kwa kuomba neema za Roho Mtakatifu, zituwezeshe kuelewa hata kwa kiasi kidogo, maana ya upendo huu wa Mungu, usiokuwa na kipimo. 








All the contents on this site are copyrighted ©.