2015-10-19 15:27:00

Fides yatoa takwimu za Kanisa Katoliki 2015


Jumapili iliyopita Oktoba 18, 2015, ambayo ilikuwa ni Jumapili ya Mission,Shirika la Fides, ambalo ni Wakala wa habari za Kanisa Katoliki, kama ilivyo kawaida yake kwa siku hii, ilitoa picha ya jumla ya hali halisi ya Takwimu za Kanisa Katoliki,  kwa kutoa baadhi ya takwimu muhimu za Kanisa Katoliki  duniani.  Taarifa inasema, Takwimu mpya zinalinganisha na takwimu zilizoandikwa katika kitabu cha Takwimu za Kanisa zilizofanyiwa kazi 31 Desemba 2013,  kuhusu Idadi ya waamini Wakatoliki, miundo yake ya kichungaji, vitengo vya huduma za  afya, elimu na msaada. 

Idadi ya watu duniani
Desemba 31, 2013, idadi ya watu duniani alikuwa 7.093.798.000, kukiwa na ongezeko la la  70,421,000 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Aidha Takwimu zinaonyesha kwamba Kibara kumekuwa na ongezeko kama ifuatavyo Asia (+mil27) na Afrika (+mil23), ikifuatiwa kutoka Marekani (+mil17), Ulaya (289,000) na Oceania (683,000).

Idadi ya Wakatoliki
Kwa upande wa Idadi ya Wakatoliki inaonyesha kwamba  Desemba 31, 2013 idadi ya Wakatoliki ilikuwa  1.253.926.000.  Ongezeko hili kiibara kwa mwaka jana, ni kama ifuatavyo,  Amerika (+ milioni 15,051,000) na Afrika (+7,637,000), ikifuatiwa na Asia (+2,161,000), Ulaya (285,000) na Oceania (171,000). Kiasilimia ongezeko la Wakatoliki kibara imekuwa  Afrika (0.29%), Marekani  (0.38%), Asia (0.03%), Ulaya (0.03&) Oceania kumekuwa na upungufu kidogo wa asilimia  -0.01%.
Maaskofu
Idadi ya Jumla ya Maaskofu Katoliki ulimwenguni, iliongezeka kwa Maaskofu 40, na kufikia 5,173, Maaskofu wa Majimbo wakiongezeka zaidi ya Maaskofu kutoka Mashirika ya Kitawa. Maaskofu wa jimbo wakiwa  3,945 (28); Maaskofu Kidini ni 1,228 (12 zaidi). Ongezeko la Maaskofu wa jimbo mabara yote isipokuwa Australia na Pasifiki ambako kulikuwa na upungufu wa Maaskofu -5:  huku kukiwa na ongezeko barani Amerika ya Kaskazini kwa 16, Asia 8, Afrika 3 na Ulaya 6. Maaskofu kutoka Mashirika ya Kitawa ikiwa  Afrika 2,  Amerika ya .Kaskazini 1, Asia 6, Ulaya 3.
idadi ya Mapadre
Idadi ya jumla ya idadi ya Mapadre ulimwenguni  iliongezeka kwa Mapadre wapya  1,035 kwa takwimu za mwaka uliotangulia hadi  kufikia Mapadre 415,348. Barani Ulaya kukiwa bado na upungufu mkubwa wa Mapadre  2283, lakini kukiwa ongezeko barani  Afrika la Mapadre 1693, A.Kaskazini 188 na Asia 1440. Mapadre wa Jimbo 971, wameongezeka na kuifanya idadi ya jumla  ya Mapadre wa Jimbo kuwa  280,532. Na Mapadre Watawa 64 wakiwa na hivyo  kuifanya jumla yao kuwa Mapadre Watawa 134,816.

Mashemasi wa kudumu : kuna mashemasi wa kudumu 1,091 walioongezeka  na kuifanya idadi ya Mashemasi wote wa kudumu kuwa 43,195, wengi wapya wakiwa barani Amerika na Ulaya. Idadi ya mashemasi wa Jimbo wakiwa 42.650  na waliobaki ni wa mashirika ya kitawa na walei. 

Watawa wanaume na Masista: taarifa inasema wingi wa watawa wasiokuwa mapadre kujiunga ilipungua ikilinganisha na miaka ya nyuma, kukiwa na watawa wapya 61 tu na hivyo kuifanya idadi ya wtawa wote waiso Mapadre kuwa 55,253. na pia watawa wa kike waliojiunga imepungua kwa mwaka huu wkaiwa 8,954 na hivyo kuifanya idadi ya masista wote kuwa 693,575. Wakati huohuo idadi ya wanachama katika Taasisi za Walei pia kidunia walipungua wanachama walei 59 , ikilingnaisha na mwaka uliopita. Na kwa upande wanachama katika taasisi za wale za Kike kukiwa na ongezeko la  walei wapya 747 waliojiunga na kuifanya idadi yote kuwa 23,955.  

Na kwamba, kumeongezeko Majimbo mapya ya  Kanisa 8  na kufikia Majimbo 2989. Barani Afrika kukiwa kumeundwa  majimbo mapya mawili.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.