2015-10-16 14:33:00

Maisha hasi ya utoto yanaweza kuwa chanzo cha tabia mbaya


Ripoti ya Chama cha Ulinzi wa Mtoto “ kinachojulikana kwa jina la “ suala ya maisha na kifo” inaonyesha kwamba,  uzoefu hasi  wa utotoni, huathiri maisha yote ya mtu, kitabia na kiafya. Maisha mabaya ya utotoni yanaweza kuwa chanzo cha  tabia mbaya za mtu baadaye anapokuwa mtu mzima,na huongeza asilimia kubwa ya vifo vya mapema, myumbo wa maisha, utumiaji wa  madawa ya kulevya,  kutopenda shule  na kuwa na  tabia ya  hasira na fujo. Yote haya huchangia kuchochea migogoro, na kuendeleza mzunguko wa umaskini na kudumisha ukosefu wa utulivu kwa jamii nzima.

Ripoti hiyo imefanya rejea katika takwimu za Syria zinaonyesha kwamba,  wavulana kati ya miaka 13 na 17 wamekuwa na uwezekano mkubwa wa kujeruhi  au kuua kwa mara nne zaidi wakilinganishwa na wenzi wao wasichana katika umri huo. Na kwamba uwezekano huu wa kujeruhi au kujeruhiwa  wakiwa mbali na wazazi au familia zao , hasa hutokana na matatizo ya kukosa upendo ndani ya familia na msaasa wa kibinadamu kwa watu waliokaribu nao , na hivyo kusababisha matatizo zaidi ya muda mrefu.

Ripoti hiyo inaonya kwamba bila uwepo wa juhudi za kisiasa, na uwezo wa kuhakikisha kwamba, watu wote wanakubalika na ubinadamu wao kuheshimiwa na pande zote zinazopingana, si rahisi kupunguza  athari za vita kwenye uwanja wa ubinadamu.

Kwa maoni hayo Ripoti imetaja hatua muhimu za kuchukuliwa kwa ajili ya  kujenga moyo wa  ubinadamu  kwa mtu  tangu utotoni kwamba,

• Serikali na taasisi zisizo za kiserikali,  wote wanapaswa kujua kanuni za sheria ya kimataifa ya kibinadamu na jinsi mtu anavyopaswa kuwajibishwa iwapo atapatikana na hatia ya kukiuka haki za biandamu.
• Vyama vyote  vya kisiasa vinapaswa kutoa kipaumbele kwa usalama, ustawi na ulinzi wa watoto katika hali zote za kidharura.
• Serikali na wafadhili binafsi lazima kukusanya  fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha ufanisi katika kazi za ulinzi wa watoto katika hali ya dharura.
• Watendaji wote katika  huduma za kibinadamu wanapaswa kushirikiana katika mawasiliano ili kuhakikisha kuwa mahitaji  ya watoto na maoni  yao pia yanapewa uzito. .
• Na kwamba watendaji wa huduma ya ubinadamu na wafadhili,  kuweka ushiriki wa watoto katika viituo mkakati kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano na watu wazima walioathiriwa na migogoro,  na kutoa tathmini ya mahitaji, na wakati huo huo, kukuza upatikanaji wa huduma kwa watoto kwa njia za mawasiliano. SOS Mila Italia imetaarifu.








All the contents on this site are copyrighted ©.