Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Duniani, ambayo ni kila tarehe 12 Oktoba , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki moon ametoa wito wa kutambuliwa kwa juhudi za jamii, kubwa na ndogo, ambao kwa hekima yao, ushirikiano wao wa thamani na maarifa kwa maisha , waliweza kukabiliana na majanga. Ameandika Katibu Mkuu wa Umoja Bwana Ban ki-Moon katika ujumbe kwa maadhimisho ya mwaka huu, akilenga katika kujenga nguvu ya maarifa ya jadi, asili.
Hotuba yake imetoa mfano mzuri, wa kimbunga Pam kilichotokea katika bahari ya
Pasifiki mwezi Machi, jinsi ambavyo hapakutokea maafa makubwa kwa watu kutokana
na jinsi makazi yao wameyajenga katika mtindo wa kijadi uliozingatia hali halisi za
hewa katika eneo hilo na hivyo tufani au kibunga vinapotokea , hakuna madhara makubwa
kwa maisha ya watu wengi. Ban amesema, "maarifa ya jadi na hekima za wazawa ni msingi
muhimu, kwa jamii nyingi zinazopendelea kuishi kwa amani na katika kukabiliana na
matukio asili kama machafuko ya hali ya hewa, ongezeko la joto na kupanda kwa bahari."
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliendelea kubainisha kwamba, juhudi za Umoja wa Mataifa
akisema, mfumo wa kazi kwa ajili ya kupunguza hatari za maafa,, unatambua umhimu wa
ushiriki wa jamii katika ngazi zote. Pia imesisitiza jinsi maarifa ya jadi yanavyoweza
kusaidia elimu ya kisayansi katika usimamiaji wa majanga. Kujenga ujasiri na majanga
pia ni kipengele muhimu katika Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo ni mwongozo
wa juhudi za watu duniani katika kukomesha umaskini na kukuza ustawi wa pamoja katika
dunia ya afya ifikapo mwaka 2030.
Aidha Jumapili iliyopita, Mkuu wa Kanisa la Ulimwengu, Papa Francisko , aliikumbuka
Oktoba 13, Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa, akisema, "Ni lazima kuwa na utambuzi
kuwa madhara ya majanga, mara nyingi husababishwa na kiburi cha binadamu katika
hudumia mazingira. Papa alieleza hilo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, aliyosali
mbele ya mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro. Papa alisema ni muhimu kwa kila mmoja wetu kujiunga katika juhudi za kimataifa
na serikali za mitaa kwa ajili ya kupunguza maafa, kuwa na ujasiri mkubwa katika
kupambana na maafa kwa njia ya kuhuisha elimu mpya na ile ya jadi kwa makini hasa
kwa watu walio hatarini zaidi.
All the contents on this site are copyrighted ©. |