2015-10-09 14:57:00

Francisko: uzushi,wivu na mitego hutoka kwa Shetani.


Tafasiri mbaya za makusudi kwa  yaliyo mema,  na uzushi wa mambo kwa sababu ya wivu, pamoja na kuwawekea wengine mitego ya kwa nia ya kuwaangusha katika dhambi ni utendaji wa kishetani. Baba Mtakatifu alionya Ijumaa hii, katika mahubiri yake ya wakati wa Ibada ya Misa ya asubuhi katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta, ambamo alihimiza waamini kutambua hayo na kuwa na ujasiri wa kukabiliana nayo, kwa kujenga moyo imara katika kutambua majaribu yanayowekwa mbele yao-

Maelezo ya Papa yalijikita zaidi katika somo la Injili , ambamo Yesu anamfukuza pepo mbaya na mtu aliyefika kumsikiliza na mtu huyo kuwa mwema, na kukaa miongoni wa watu, akimsikiliza na akitambua  mamlaka ya Yesu. Lakini katika kundi hilo la watu ,  Papa alibainisha kwamba, kulikuwa na wengine waliofika kumsikiliza Yesu kwa nia za kutaka kutoa kutafsiri kinyume maneno ya Yesu na mitazamo yake, wakiwa dhidi ya Yesu. Na wengine walikuwa ni watu waliomwonea Yesu wivu tu , na wengine walishikilia mafundisho ambayo wenyewe walishindwa kuyaishi na  wengine waliogopa ukali wa utawala wa Kirumi na mauaji; Na hivyo kwa sababu nyingi walikataa kukiri mamlaka aliyokuwa nayo ya Yesu ka hofu za kushutumiwa pia, kama ilivyokuwa katika tukio hili la Ysu kumtoa pepo mtu. Yesu anashutumiwa kwa maneno ya ajabu kama  anamfukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. Na  walimfananisha na  mtu mwendawazimu, au kama mchawi,daima walipenda kumjaribu na kumtega , ili wapate  kumshutumu.

Homilia ya Papa , illiendelea kuwahimiza watu kuomba neema ya kutambua wakati wanapowekwa katika mitego na majaribu. Watoe jibu linalofaa kwa ujasiri bila kuyumbishwa.  Na utambuzi huu hupatikana kwa kuchagua njia sahihi itokayo kwa Mungu na si kutembea katika njia ya ya mwovu yenye majaribu na udanganyifu mwingi. Papa alieleza na kuwaasa Wakristo kwamba, si  rahisi kwamba watu wote ni wema, ni lazima kuwa na utambuzi wa mambo , kutazama vizuri  watu hao wanatoka wapi na mzizi wao ni katika nini.

Baada ya kueleza kilichotokea katika tukio hili, Papa alionya dhidi ya mwovu shetani, kuupumbaza utambuzi na akili ya kuwa macho na mwovu, kwa sababu katika safari ya imani, mwovu haendi mbali na mtu mwema. Mwovu hukaa karibukaribu akisubiri hatanafasi ndogo ijitokeza ili amwingine tana mtu. Ndiyo maana Papa alisema , majaribu au vishawishi vya roho roho mbaya hujirudia mara kwa mara , mwovu hachoki kamwe kumzungukia mtu. Kama amepigwa mateke nje, kwa uvumilivu hutulia kando akisubiri kurudi tena ndani. Na iwapo anapata nafasi ya kuingia basi humwangusha mtu vibaya zaidi.  

Papa aliendelea kuonya kwamba, kupumbaza utambuzi na dhamiri , ni uovu mkubwa, kwa kuwa wakati roho mbaya anapoweza kusinzisha dhamiri, hapo hushangilia ushindi wake  halisi, na kuwa bwana wa dhamiri,akiamurisha kutenda anavyotaka. Na hapo huwa mwanzo wa matatizo yote na kila dhambi ambamo mtu anaona haki kuishi kwa ajili ya mambo ya dunia hii akiongozwa na roho mbaya.

Papa ametaja njia ya kukabiliana na roho huyu mbaya , daima ni mtu kuyachunguza maisha yake ya kiroho. Papa amesisitiza mawili katika hili kuwa ni kuwa macho na kuwa na utambuzi. Kanisa daima linatushauri kuchunguza  dhamiri za maisha yetu binafsi kila siku kabla ya kuifunga siku: kujiuliza nini kilichotokea leo katika moyo wangu, na  kwa nini? Ni kujiuliza je kulikuwa na mapepo mabaya waliotaka kuniingia kupitia kwa marafiki zangu? Je nami nimekuwa pepo mbaya kwa wezangu?  Papa amehimiza  utambuzi wa nia kwa kila tendo, hata katika kutoa  maoni, maneno na mafundisho,mahali popote na wakati ni kujiuliza  kwa nini nasema hivi? Kutambua na kuwa macho, isiwe ili mradi kwa kuwa huko ni kujidanganya, ni kujiingiza katika mitengo na vishawishi vya kupendezwa na mabaya. Papa aliomba kwa Bwana : neema ya  utambuzi na neema ya  ujasiri.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.