2015-10-08 16:20:00

Baba Mtakatifu amezikabidhi kwa Mama yetu wa Rosari familia zote


Jumatano wakati wa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni , aliyoitoa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa Francisco , aliwakumbusha wote kwamba ,  tarehe 7 Otoba  Mama Kanisa, hufanya kumbukumbu kwa  Mama yetu wa Rozari. Na hivyo katika maelezo yake Papa, alizikabidhi familia zote  duniani chini ya ulinzi wake na pia Mkutano wa Sinodi juu ya familia. Na alitoa mwaliko kwa waamini wote , kumwiga Mtakatifu Yohana Mtume, kumpokea Mary katika nyumba zao na wamwachie nafasi katika maisha yao ya kila siku,  kwa sababu huduma yake ni ya mzazi, chanzo cha utulivu na nguvu  za kusonga mbele.

Baada ya maelezo hayo , Papa aliwageukia  vijana, wagonjwa na maarusi wapya akisema , kwenu wapendwa vijana, tumaini lililo ndani ya Moyo wa Maria , na liweze kuwapa ujasiri thabiti mbele ya uso uchaguzi  wa maisha. Na kwa  wapendwa wagonjwa alisema, nguvu za Mama Maria chini ya Msalaba wa mwanae, ziandamane nanyi wakati wa vipindi vigumu zaidi katika maisha . Na kwa Maarusi wapya , aliwaombea, huruma ya Kimama, iliyompokea Yesu tumboni mwake iwasindikize katika maisha yao mapya ya kifamilia ambayo wameyaanza mara.

Ibada ya sala ya Rosari ilianzishwa tangu karne a kumi na Tatu na Mapadre Wadominikani . Na tarehe 7  Oktoba 1913,   Mtakatifu Papa Pius X , aliitangaza tarehe hiyo kuwa  Ni siku ya Maadhimisho ya Kanisa, kama  Sikukuu ya Rozari. 








All the contents on this site are copyrighted ©.