2015-10-07 10:41:00

Muhtasari wa majadiliano ya Sinodi katika kikao cha Tatu cha Jumanne 6 Oktoba 2015


Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican,Askofu Mkuu Claudio Maria Celli, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Jamii, na Kardinali Paul Andrè Durocher , walitoa kwa wanahabari muhtasari wa majadiliano yaliyofanyika katika kikao cha Sinodi inayoendelea katika Ukumbi mpya wa Sinodi ulioko ndani ya Vatican. Wanahabari walitahadharishwa tangu mwanzo kwamba, hakuna marekebisho yaliyofanyika katika Mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ndoa, kama alivyoeleza Papa Francisko katika hotuba yake ya mapema asubuhi, wakati wa kikao cha Tatu cha jumla cha Sinodi hii ya  kawaida juu ya juu ya familia.

Padre Federico Lombardi pia alikumbusha kwamba, majadiliano yanayoendelea katika ukumbi wa Sinodi, ni mwendelezo wa Sinodi ya  mwaka 2014, wakati ambamo Mafundisho Katoliki juu ya ndoa yalibaki kama yalivyo. Hapakuwa na marekebisho. Aliendelea kurejea hotuba ya  Papa Francisko, ilichofuatiwa na kazi za vikundi. Kwamba,  Papa  amerejea katika nyaraka tatu zinazohusiana na Sinodi za awali  na hotuba mbili za Papa ile  ya kufungua na kufunga kikao, na hivyo akawataka wanahabari wasichanganye na  maoni yanayotolewa wajumbe  nje ya vikao vya Sinodi.

"Aliwataka wanahabari wasishinikizwe au kupunguza upeo wa kazi za Sinodi hii, kama vile tatizo pekee linalotafutiwa ufumbuzi ni wanandoa kutalakiana na kuoa au kuolewa tena.  Hivyo Padre Lombardi akaendelea kukumbusha pia  kuna  matatizo na masuala mengine ambayo yamependekezwa yajadiliwe katika Mkutano huu wa Sinodi , kama ilivyotolewa katika rasimu  ya kazi "Instrumentum Laboris" katika mtazamo mpana zaidi.

Nae Askofu Mkuu Claudio Maria Celli, Rais wa Tume ya Sinodi kwa habari, akijibu waandishi wa habari, yeye pia alifafanua kwake yeye , hotuba ya Papa ya asubuhi ,  iliyorejea  nyaraka za rejea za  mijadala ya Sinodi  za nyuma na hotuba zake mbili, kufungua na kufunga ,akisema  ilikuwa ni kuweka mtazamo wazi juu ya mwelekeo wa Kanisa ,  kwa kazi za Kichungaji katika kukabiliana  hali halisi za tatizo la talaka. Inabidi hivyo daima kama alivyoeleza Papa katika hotuba yake , mapema asubuhi hii kwamba,  Sinodi  si kituo pekee cha rejea katika matatizo ya wanandoa, bali  ni kati tu ya rejea nyingine.

 Aidha, Padre  Lombardi,  alisema majadiliano ya sinodi yanafanyika katika  lugha sahihi  ya Kanisa, ili kuepuka hisia ya hukumu hasi dhidi ya hali na watu.  Na kwamba Papa Francisco, amekuwa daima akisisitiza haja ya kusaidia wote wenye ndoa kukua na kukomaa katika imani na katika ndoa, hasa kwa vijana wanandoa  kugundua upya uzuri wa upendo na mahusiano yao ya kama wapenzi na wanandoa. Pia  amekuwa akitaja mara kwa mara ushahidi wa familia ya kimisionari  kuwa ni muhimu kwa maisha ya Kanisa. Na pia amekuwa akifanya rejea kwa yanayojitokeza kwa familia zinazoishi katika mazingira magumu, janga la umaskini katika familia, na vurugu zenye kuathiri familia yenyewe, pamoja na  janga la ajira kwa watoto, hatma ya wakimbizi na wahamiaji na mateso dhidi ya Wakristo. Aidha  alilenga pia juu ya suala la watu wenye tabia za ushoga akisema  wao ni sehemu ya Kanisa, lakini ni wazi,kanisa linawapokea kama walivyo lakini muungano wa  sakramenti ya ndoa unabaki kwa mwanamke na mwanaume, msingi wa familia  na jamii kwa ujumla. 








All the contents on this site are copyrighted ©.