2015-09-30 16:55:00

Katekesi ya Papa aelezea kwa ufupi ziara yake ya kitume ya Quba na Marekani


Vatican Radio:  Papa alianza katekesi yake akiwasimulia kwa ufupi juu ya ziara yake ya kichungaji ya huko Quba na Marekani, ambayo alisema ilitokana na utashi wa kuudhuria mkutano wa Dunia wa Familia katika mpango wa Filadelfia. Pamoja na safri hiyo ilimwezesha kuunganisha matembezi ya Marekani katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa akitokea Quba.Bado alitoa shukrani nyingi kwa Rais Castro, Rais Obama, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa makaribisho yao.Na pia kuwashukuru maaskofu ndugu zake na wasaidizi wao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya upendo kwa kanisa.

Papa alisema alivyofika huko akiwa ni mmisionari wa huruma , katika nchi nzuri yenye utajiri wa asili , utamaduni na imani.na kusema , Huruma ya Mungu ni kubwa zaidi ya majerah, vurugu za kila aina ya itikadi zote, na kwa namna hiyo alipata kuwasalimia watu wote wa Quba wakiwa wanaadhimisha miaka 100  ya kutangazwa Bikira Maria wa Upendo wa huko Cobre kuwa msimamizi wa nchi hiyo.Papa alisema ya kwamba alipata kushirikiana na watu hao wakiwa na matumaini  kwa kutilimilizika unabii wa  Mtakatifu Yohane Paulo wa II  alipoiombea nchi ya Quba ifungulie milango  katika ulimwengu na ulimwengu pia ufungulia milango Quba.

Nchi hiyo haitafungiwa tena, wala kunyanyaswa katika umasikini, bali  watapata uhuru na utu, alisema Papa. Aidha alibainisha ya kwamba hiyo ndiyo njia inayofurahisha mioyo ya vijana wa Quba.Papa alisema aliwatia moyo wote na zaidi kwa mapadre , watu waliowekwa wakfu, wanafunzi na familia. Na kwa nguvu ya roho mtakatifu , na kwa maombezi ya Bikira Maria mtakatifu  ili aweze kukuza mbegu walizopanda.Papa alieleze juu ya ziara yake katika  maeneo matatu ya Washington, New York na  Philadelphia, na kwamba alivyokutana na viongozi wa siasa ,pia  raia  maaskofu na watu waliowekwa wakfu, masikini na watu waliowekwa pembezoni nawakumbusha jinsi ya kudumisha utajiri wa nchi na watu na pia urithi wa kiroho na maadili.

Aliwatia moyo waendeleze na kujenga jamii kwa uamainifu ambao ndiyo msingi , kwani binadamu wote wameumbwa na Mungu na wote ni sawa ambao wanahitahitaji haki sawa, maisha sawa, uhuru, na kupata  furaha.Maadili hayo yanapatikana katika injili ambapo Papa alisema alipata kumtangaza baba wao wa Taifa Junipero Serra mfransiskani na muhubiri mkubwa wa Kalifornia, ni baba aliyeonyesha njia ya furaha, ya kwenda kukutana na kushirikisha wengine upendo wa Kristo. Papa aliendelea kuwaeleze juu ya ziara pia ya new York na sehemu zote alizopitia ambapo alipata pia kuwatia moyo katika kujenga na kudumisha maendelea na hasa wito wa kutafuta amani na ulazima wa utunzaji wa mazingira

Aidha papa alielezea  jinsia alivyotoa wito juu ya kuacha na kuzuia ukatili dhidi ya makabila madogo na dini na pia  uraia.vilevile alivyopata fursa ya kusali katika eneo la kumbukumbu ya Ground Zero pamoja wawakilishi wa madhebu mengine pamoja na ndugu na jamaa wa wathirika wa tukio la kigaidi la 2001 na kwa ajili ya amani  ya kuomba amani aliazimisha  ibada Takatifu katka jengo la Madison Square Garden. Papa Pia alisema jinsi alivyokuana na kuona huko New York na Washington  matendo ya huruma na elimu, ambayo yatolewayo na jumuiya katoliki .

Papa alimalizia akielezea  ziara yake ya mwisho katika mkutano wa Dunia wa familia ambao ndiyo ulikuwa mtazamo wa  upeo wake ambao  papa aliufananishana prism namna ya kutaja familia.Alisema familia ni Muungano unatoa matunda kati ya mwanaume na mwanamke, ambayo ni jibu lenye kuwa na changamoto mbili katika dunia ya leo akisema :Mgawanyiko na viwango , ni mambo hayo mawili yanaoishi kwa pamoja na kusaidiana pamoja , na pia kuunga mkono katika mfumo wa kiuchumi katika ulaji. Familia ni jibu kwa sababu ni kiini cha jamii ambayo utoa mizani inayopima ukubwa binafsi na ule wa jamii,na wakati huo inaweza uwa mfano wa usimamizi endelevu  wa mali na rasilimali za  viumbe.Familia  ni wakala mkuu wa viumbe na mazingira kwa ujumla.kwasababu ni somo la kwanza katika jamii  ambayo inatoa kanuni mbili zenye msingi , yaani ile wa  ustaarabu wa binadamu katika ardhi, na pia ya  kanuni ya kushirikiana katika kuzaa.

Papa anasema kwamba   katika utu kwenye  Biblia unaonyesha picha  ya kwanza ya binadamu wanandoa, umoja  na uzazi ambao uliwekwa na Mungu katika bustani ya Dunia, ili kuilima na kutunza. Shukrani  zake zilimwendea Askofu Mkuu wa Philadelphia kwa kazi kubwa waliyo ifanya ya maandalizi ya tukio hilo la Mkutano wa Dunia wa Familia .Kwa mtazamo wake alisema haikuwa  kwa bahati mbaya  bali ni kwa maongozi ya Mungu ujumbe na ushuhuda wa Mkutano wa dunia wa familia kufanyika muda huu katika nchi ya Marekani, nchi ambayo karne iliyopita imepiga  maendeleo kwa kiwango cha juu kiuchumi na kiteknolijia bila kukana mizizi yake ya dini. Papa akasema kwamba. kwa mzizi hiyo sasa wanaombwa  kuanza upya na familia kufikiri na kubadilisha miundo ya maendeleo , kwa manufaa ya jamii nzima ya kibinadamu.








All the contents on this site are copyrighted ©.