2015-09-28 14:04:00

Afrika Kusini: Wavuvi kumi wafamaji katika machafuko ya bahari


Kwa mujibu wa Mtandao wa Mamlaka ya Kitaifa ya Bandari Afrika Kusini(TNPA),  Wavuvi kumi wamefariki dunia na watatu bado hawajulikani walipo baada ya mtumbwi wao kukumbukwa na machafuko ya bahari Jumapili usiku. Msemaji Craig Lambioni wa NISRI ameripoti na kunukuliwa na allafrica.com

Taarifa hiyo inasema, boti nyingine ilifika katika tukio hilo haraka na  kuweza kuwaokoa wavuvi tisa , lakini wengine kumi walikuwa tayari  wamefariki. Mtumbwi huo uliokumbwa na mawimbi makubwa, ulikuwa na jumla ya wafanyakazi 21. Machafuko ya bahari yanatajwa kutokana na upepo uliokuwa ukivuma tokea Kusini Mashariki.  Lakini hali bahari ilianza kutulia wakati wa operesheni ya utafutaji na uokoaji.

Pamoja na utulivu wa bahari, juhudi za kuwapata wavuvi wengine watatu bado kufanikiwa Radio ya  mawasiliano ya huduma za Majini  "Telkom Maritime Services", imethibitisha taarifa hii.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.