2015-09-26 12:23:00

Ujumbe wa Papa Francisco kwa New York :” Mungu yu hai katika miji yetu”


Ijumaa, kama sehemu ya ratiba yake katika kulitembelea jiji la New York,  Baba Mtakatifu aliongoza Ibada ya Misa katika Bustani ya Madison , ibada iliyohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la New York, wakiwemo Maaskofu, Mapadre Watawa wakiongozwa na Askofu Mkuu Kardinali Timothy Michael Dolan wa Jimbo Kuu la New.

Papa katika hotuba yake aliyoitoa katika lugha ya kihispania na kutafasiliwa kwa Kiingereza, pia aliwakumbusha  kutosahau kuwahudumia watu maskini na wahitaji wa mji huo.

Papa Francisco aliendelea kuzungumzia wajibu waamini Wakristo katika kutumikia amani na kuwa mashahidi na wataalamu wa ujenzi wa amani, kuthibitisha katika maisha yetu, mfano ukuu wa Kristo , aliyetangazwa na Nabii Isaya kwamba ni Mfalme wa amani. Aliwaambia wote waliokuwa wakimsikiliza, “Nendeni  kwa watu wengine na kuwashirikisha  habari njema kwamba Mungu, Baba yetu, anatembea kando yetu. Papa Francis aliyaambia maelfu ya watu hasa vijana walioshiriki katika Ibada hiyo. Na kwamba  Yeye Kristo  Bwana, hutuopoa na maovu yote ya maisha , hali ya utupu na upweke na ubinafsi ,na huturejesha katika shule ya kukutana na wengine. Yeye  hutuondoa kutoka dhambi ya ushindani na ubinafsi, na kufungua mbele yetu njia ya amani. Amani hiyo inayozaliwa kwa kuwakubali wengine kwa  amani iliyojaza mioyo yetu, na kutusukuma kutazama wahitaji zaidi ndugu zetu na dada.

"Mungu," alisema Papa Francis, "anaishi katika miji yetu: Kanisa linaishi katika miji yetu, na anataka kua kama hamira ilivyo ndani ya unga. Ana hamu ya kumwambia kila mmoja , na kusimama kando ya kila mtu, kama Yeye anaye tangaza maajabu ya, Mungu, Mungu  mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.  Papa alieleza na kunukuu tena aya kutoa Isaya "Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru kuu, "- na sisi wenyewe ni mashahidi wa mwanga."

Homilia ya Papa pia ilionyesha kutambua kwamba kuishi katika majiji si jambo jepesi kwa kuwa ni kukutana na watu wa kila tabaki na hata kuna ubaguzi wa kuwaweka watu wengine daraja la juu na wengine daraja la chini. Lakini kwa utambuzi kwamba Kristo  pia anatembea mitaani , na kwamba ni sehemu ya watu wanaishi katika maisha magumu na sehemu ya mpango wake wa wokovu kwetu, tunajazwa na Tumaini . Tumaini linalotuweka Huru dhidi ya nguvu na mashinikizo yote yanayotaka kututenganisha na kutojali maisha ya wengine katika maisha haya ya mjini. 








All the contents on this site are copyrighted ©.