2015-09-26 10:40:00

Hotuba ya Papa kwa Umoja wa Mataifa: dunia yadai ufumbuzi wa haraka na fanisi


Ijumaa 25 Septemba 2015, Baba Mtakatifu Francisko aliutembelea Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa. Hotuba yake ilisisitiza  kwamba, dunia  kwa nguvu,  inadai serikali zote kuwa na nia na utendaji thabiti, kutekeleza maamuzi yanayotolewa na wote .

Papa Francisco amekuwa ni Papa wa nne  kutembelea Umoja wa Mataifa. Na ametembelea kama sehemu ya tukio la Mkutano Mkuu wa 70, na pia kama kumbukumbu ya kupita miaka  50  ya hotuba ya kwanza  ya Papa katika Umoja huo,  iliyotolewa na Mwenye Heri Papa Paulo VI mwaka  1965.  Papa Yohana Paulo II aliutembelea  Umoja wa Mataifa mara mbili mwaka 1979 na 1995, na Papa Mstaafu Benedikto XV1  alikwenda mwaka 2008.

Hotuba ya Papa kwa ujumla imetazama umuhimu wa Umoja wa Mataifa, maovu yanayotesa dunia leo hii kama unyonyaji, vita, umaskini, madawa ya kulevya na kutoa wito wa  kutafuta jawabu la  haraka na fanisi. Papa alisema "napenda kuongeza sauti yangu kwa wale wote wanaotamani, ufumbuzi wa haraka na ufanisi kukabiliana na matatizo haya yanayoirarua dunia".

Katika hotuba hii , iliyopigiwa makofi mara kwa mara , Papa alizungumzia kwa nguvu zote,  haja ya kujenga muafaka imara wenye kuvunja hila zote za utengano na kukosekana kwa usawa kunako umiza binadamu. Papa alisema ni kuanzia na  taasisi za Umoja wa Mataifa wenyewe,  kuwa na sheria thabiti zinazo zingatia sababu za  kuanzishwa  na kudumisha mafanikio  muhimu ya  pamoja kama uboreshaji wa haki za wengi katika neema ya uhuru na ulinzi wa heshima ya utu mwa mtu. Na aliongeza kusema, "Mafanikio haya yote ni wanga unaomulika dhidi ya giza la machafuko yanayosababishwa na ulafi, tamaa na ubinafsi pamoja".

Papa akirejea lengo la kuundwa kwa Umoja wa Mataifa kwamba ni kudumisha  haki, aliwakumbuka wote wale ambao wamekuwa kafara katika utume wao wa kuhudumia ubinadamu wa amani na maridhiano. Na alimtaja kati ya wengine Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani na mara mbili Katibu Mkuu wa UN,  hayati Dag Hammarskjold.

Aidha hotuba ya Papa imetaja umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika kupambana na na changamoto zinazojitokeza kama vile uhaba wa  ruzuku kwa ushiriki nchi na utekelezwaji  wa na maamuzi halisi na ya  haki. Na pia akazitaka taasisi za Kimataifa za  fedha" kuwa macho na "maendeleo endelevu ya nchi"na hasa kujiepusha na maamuzi yenye kukaba koo maoni ya watu mahalia katika kustawisha maendeleo yao,na taratibu za kupambana na umaskini wa kukithiri, kutengwa na utegemezi.  Papa alitaja haki kuwa sharti msingi la kufikia  udugu mzima  uliobora kama kiwango cha juu cha nguvu na  thabiti katika dhana ya sheria.

Na kwamba  hakuna kundi, mtu binafsi au watu wenye kujiona kuwa na  nguvu zote, wanaoweza kuruhusiwa kukanyaga heshima na haki za watu wengine au makundi ya kijamii.  Na alitazama upande wa mazingira na kusema ukweli wa sheria ya asilia ya mazingira vizingatiwe kwa sababu,  kimsingi binadamu pia  ni sehemu ya mazingira na hili linatawaliwa ina mipaka ya kimaadili, inayotaka  hatua za  utendaji wa binadamu lazima kutambua na kuheshimu mazingira.  Hivyo haribifu wowote kwa mazingira,  ni kuumiza ubinadamu pia .

Papa anasisitiza kuwa kila kiumbe kina thamani kwa jinsi kilivyo chenyewe na katika mfumo asili wa kutegemeana na viumbe wengine. Hivyo matumizi mabaya na uharibifu wa mazingira, inakuwa ni mfumo mbaya wa kutaka kujitenga na wengine, hasa kutokana na ubinafsi na nguvu ya  tamaa za kutaka kuonekana kuwa juu ya wengine na kama matokeo yake  hujenga tabaka la wanyonge na wasiojiweza katika hali za maisha. Utengano  kiuchumi na kijamii, wenye  kudhoofisha mshikamano wa jumla wa udugu wa binadamu na  hivyo inakuwa ni shambulio kubwa kwa  haki za binadamu na mazingira.
 

Papa alieleza na kusisitiza kwamba, dunia kwa nguvu inataka serikali zote ziwe na nia madhubuti na vitendo thabiti. Ni lazima kuhifadhi na kuboresha mazingira li  kuondokana na mijeledi ya  kijamii na kiuchumi yenye kujenga  utengano, wenye kuathiri wengi , mijeledi kama ya "usafirishaji haramu wa binadamu", "biashara haramu ya silaha na madawa,  ugaidi na uhalifu wa kupangwa wa kimataifa.

Papa alitoa ombi la kutositisha mchakato wa kutazama hali halisi katika maisha ya kijamii, ili kuchukua hatua zinazo stahili katika za kukabiliana na wanachopambana nacho wanaume na wanawake, ambao mara nyingi wanaishi katika umaskini na wenye kupokonywa haki zao kama binadamu.  Ni lazima  kuwashirikisha watu mahalia katika utendaji wa shughuli zote kwa stahili ya hatima yao wenyewe na katika ushirika na wanadamu wengine.Katika  Mshikamano wa maendeleo ya binadamu na zoezi kamili ya utu wa binadamu lisilo na mbadala. Wakati huo huo - aliendelea - viongozi lazima kufanya kila linalowezekana ili kila mtu aweza kupata mahitaji yake msingi ya kihali na kiroho  ili kudumisha hadhi ya utu wake  na kuunda familia, katika misingi yake asilia  kama kiini  cha msingi wa maendeleo yoyote ya kijamii.


Papa ametaja mahitaji matatu katika  kiwango msingi cha nyenzo ya utu wa binadamu kihali kwamba ni kuwa na makazi yaani nyumba ni, kazi na ardhi; na pia anahitaji katika ngazi ya kiroho: uhuru wa roho, ambao hautangamani na  uhuru wa dini, haki ya kupata elimu na haki nyingine za kiraia . Papa alizungumzia pia juu ya  ardhi, kama haki ya  kuishi na haki ya uwepo kwa maumbile yenyewe.

Na kwamba ulinzi wa mazingira na mapambano dhidi ya ubaguzi, unahitaji kutambua sheria asili ya maadili iliyoandikwa katika maumbile yenyewe ya binadamu, ambayo ni pamoja na tofauti ya asili kati ya mwanamke na mwanaume (cf .. Msifiwa ndiyo, 155) na heshima  kwa maisha katika hatua zake zote.

Bila ya kutambua  asili hii, suala la kupuuzia mipaka ya maadili mipaka - aliendelea Papa, huleta hatari  za mfuko wa  vita, dhuluma, rushwa, uendelezaji wa kiitikadi ukoloni, maisha yasiyo kuwa ya kawaida, yenye kukosa heshima kwa  utambulisho a watu wageni , kukosekana kwa uwajibikaji.  Inapaswa kukumbukwa kwamba, vita ni kukanusha usawa. "Vita ni kunyimwa haki zote na uchokozi makubwa kwa ubinadamu na  mazingira

Hivyo, kuna haja kwa dhamira hii,  kuepuka vita kwa njia ya mazungumzo kama njia Mkataba wa Umoja wa Mataifa, katika  uwazi na ukweli kwa ajili ya amani na si kwa nia chinichini zilizoficha nia tata. Aidha Papa alikemea kuenea kwa silaha akisema ,  "hapana kwa silaha, hasa zile zenye kuleta maangamizi kwa wengi. Mwandamizi wa Petro alieleza na kuonyesha  kuridhishwa na  moja kwa makubaliano ya hivi karibuni juu ya suala la nyuklia ya Iran , na tena kile alichokiita kuwa  matokeo mabaya ya uratibu wa  hatua za kisiasa na kijeshi, kati ya wanachama wa jumuiya ya kimataifa.

Papa aliigeukia migogoro dunia ya dunia kwa wakati huu, akisema "hawezi kuacha kutoa ombi lake kwa mara nyingine, kwa ajili ya  hali za uchungu katika Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na nchi nyingine za Afrika". Na alizungumzia jinsi chuki  na "wazimu" unavyo sukuma mtu kuua, kuteka wengine, kuharibu sehemu za ibada na urithi wa utamaduni. Papa aliomba jumuiya ya kimataifa kufanywa uchunguzi wa ufahamu wa watu hao wanaoendesha  vita na uharibifu. Papa Francisco aliitaja waziwazi migogoro inayoendelea  Ukraine, Syria, Iraq, Libya, Sudan Kusini na katika Maziwa Makuu.Na aòlikumbusha kwamba, katika vita na migogoro ya kisiasa watu wanaoteseka zaidi ni ndugu zetu  wanaume na wanawake, vijana na wazee, wavulana na wasichana, wasioweza kujitetea, ambao wanaugulia kilio cha mateso na kifo. Papa alieleza na kuomba Jumuiya ya Kimataifa itende wa ushupavu zaidi katika kuwalinda watu wasio na hatia. Na katika kukabiliana na majanga mengine kama  janga la madawa ya kulevya,  biashara haramu na unyonyaji wa watu", "rushwa" ambayo inajenga miundo yenye kutishia uaminifu wa taasisi.

Papa Francisko aliendelea kwa kufanya nukuu, katika hotuba iliyotolewa na Paulo VI  kwa Umoja wa Mataifa, ambamo alisema, hatari za maisha hutoka kwa  watu wenyewe.  Papa Francisco, aliendelea kuzungumzia manufaa ya wote, haja ya kujenga  udugu mzima na  kuheshimu utakatifu wa kila maisha ya binadamu. Familia ya kawaida  ​​pia lazima kujengwa juu ya uelewa wa utakatifu wa  asili uumbaji .Uelewa huu na heshima  hii zinahitaji kiwango cha juu cha hekima.

Papa ameitazama dunia ya kisasa iliyoungana kama kijiji, na  inayo endelea kupanuka kitandawazi lakini wakati huohuo pengo la migawanyiko na utengano vikizidi kukua katika jamii. Papa aliusisitiza umoja wa Mataifa kwamba, hauwezi kujiweka mbali na baadhi ajenda zinazotazama mustakabali wa dunia  kwa siku zijazo. Hivyo kwa mara nyingine , alirudia kutoa ombi lake la kuzitaka idara  na itikadi zinazohusika ,  kuhudumia kwa  manufaa ya wote.








All the contents on this site are copyrighted ©.