Baba mtakatifu Francisco Alhamisi akiongoza Ibada ya masifu ya Jioni katika Kanisa Kuu la kale la Mtakatifu Patrick, la Mjini New York, alionyesha kutambua kwamba, kanisa hilo ni matunda ya kazi ngumu ya watu wengi wake kwa waume, waliyoyatolea maisha yao mhanga bila kujibakiza katika utumishi wa kanisa. Na hivyo ameitaja kuwa ni ishara nzuri ya kazi ya wahenga, makuhani , watawa na walei aminifu wa Marekani, waliosaidia kujenga Kanisa nchini Marekani.
Papa alitazama kwa kina, jukumu lao la msingi katika ujenzi wa jamii ya Marekani,
na hivyo akatoa shukurani zake nyingi kwa makuhani na watawa ambao hasa wamejikitika
katika mipango ya elimu na lishe katika taifa la Marekani. Alieleza na kutoa mfano
wa mwanzilishi wa kwanza wa Shule Katoliki huru ya wasichana nchini Marekani, Mtakatifu
Elizabeth Ann Seton na Mtakatifu John Neumann, mwanzilishi wa kwanza wa mfumo wa
elimu Katoliki Marekani , akisema kwamba watu wengi kulipwa gharama za kafara ya ajabu
na alifanya hivyo kwa kishujaa upendo.
Lakini pia hakuogopa kutaja moja kwa moja kasoro zilizo chafua sura nzuri ya Kanisa
nchini Marekani, kashfa ya ngono kwa watoto, aibu iliyoletwa na watumishi wabovu
wa Kanisa . Papa Francisko, alikubali mateso ya wake kwa waume, na wale waliokubali
kuibeba aibu ya unyama huu uliodhalilisha ndugu hawa wanyonge katika Kanisa na
kuwaweka katika mazingira magumu zaidi ... Papa amesema anatolea sala na faraja zake
katika kwa wakati huu wa maumivu na uchungu wa moyo.
Na aliwarejea tena Mapadre na watawa wa Marekani , akiwahimiza n akuwataka wawe watumishi wema, watumikie kwa uaminifu, furaha na kuridhika katika wito wao. Wafanya kazi kwa bidii na kuyaishi maisha ya kujinyima na uaminifu kwa mujibu wa karama za waanzilishi wa jumuiya na mashirika yao kama njia ya upendeleo katika kutoa jibu kwa Upendo wake Mkuu Yeye aliyewaita katika kulitumikia Kanisa.
Kwa namna ya pekee, Papa aliendelea kutambua na kuonyesha heshima yake na shukrani kwa watawa wa kike nchini Marekani akihoji, bila wao utendaji wa Kanisa ungekuwaje hasa nchini Marekani. Alisifu kwamba, Wanawake wana nguvu, na kwa ujasiri huo, huwaweka mstari wa mbele katika kuitangaza Injili .
Alimalizia na shukurani kwa Watawa, masista na wanawake wote walioyatolea maisha yao katika kuifikisha habari njema katika kila kona ya taifa la Marekani na kwingineko duniani. "Asante Sana ", na “ninawapenda wote”.
All the contents on this site are copyrighted ©. |