2015-09-25 15:02:00

Chombo cha aina yake linacholeta sauti za watoto na vijana kwenye UN kuzinduliwa


Alhamis  24 Septemba  kwenye Umoja wa Mataifa, kimezinduliwa chombo cha aina yake kinacholeta sauti za watoto na vijana kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.  Na katika hafla hiyo  iliyoongozwa na Balozi Mwema wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, David Bekcham, Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake.

Chombo hicho cha dijitali kilichoundwa na kamopuni ya Google, kinaunganisha teknolojia ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watoto na vijana kote duniani kutuma ujumbe wao moja kwa moja kwa viongozi wa dunia. Ujumbe wa watoto hao unamulika changamoto wanazokumbana nazo nyumbani na katika jamii, zikiwemo umaskini uliokithiri, utofauti, ukatili, magonjwa na mizozo, huku wakielezea matumaini ya mustakhbali wao.

Akitoa ujumbe David Beckham  alisema "Kila mtoto ana sauti, lakini mara nyingi, hawasikiki. Wakati huu muhimu viongozi wa dunia wanapokusanyika hapa New York, sauti zao zitasikika. Dunia inapoangazia malengo mapya ya dunia, kuna fursa halisi ya kutimiza ndoto zao. Nataka ulimwengu ambapo watoto wanaweza kukua salama bila ukatili, bila umaskini na kulindwa kutokana na maradhi yanayoweza kuzuiliwa"

Ikumbukwe kwamba Siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa kupitisha malengo ya maendeleo endelevu, Umoja wa Mataifa na lengo ya ajenda 2030 ambamo kuna ya kuleta mwanga kwa maisha ya watoto na vijana , Na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson alisema ajenda mpya inatoa nuru kwa watoto na kwamba "Lengo namba 16 linajumuisha lengo dogo, na kunukuu ya kwamba."Kutokomeza manyanyaso, utumikishaji, usafirishaji haramu wa watoto na aina zote za ukatili na mateso dhidi ya watoto, likiunganishwa na mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto,  akaongeza kwamba  Kila siku wanaona  jinsi watoto wakimbizi walivyo hatarini kukumbwa na madhara. Pamoja na watoto amesema matarajio pia kwa ajenda hiyo ni kuinua fursa za ajira zenye utu kwa vijana ili nao waweze kuchangia katika ustawi endelevu wa dunia.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.