2015-09-24 12:01:00

Tanzania: serikali ipo katika jitihada za kuboresha elimu na mafunzo ya fani za usafiri


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema serikali ipo katika jitihada za kuboresha elimu na mafunzo katika fani za usafiri wa majini ili kukidhi mahitaji ya sekta hiyo kitaifa na kimataifa.Dk. Shein alitoa ahadi hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mtwara.

Taarifa kutoka Gazeti la Nipashe, lilimkariri alisema kuwa  ili sekta ya usafiri wa majini na bandari iendelee, kuna haja ya kuwa na wataalam wa kutosha na kwamba mfumo wa mafunzo na utoaji elimu ya ubaharia unapaswa kufuatwa kwa lengo la kufikia viwango vya kimataifa, kwani vyawango hivyo vitasaidia kufanya uwezo wa mabaharia wa kiatanzania kutambuluwa na kupaya ajaira si tu kwa meli za nchini tanzania bali pia meli kubwa za kimataifa.

Alisema kutokana na uwapo wa miradi ya utafutaji wa gesi na mafuta katika ukanda wa kusini ambayo inatoa fursa nyingi za ajira kwa mabaharia kupitia Bahari ya Hindi, vyombo vinavyotumika vinahitaji nguvukazi za kuviendesha na kuvihudumia ambapo Watanzania wenye ujuzi na elimu ya ubaharia, wana fursa kubwa ya kupata ajira katika vyombo hivyo. Vilevile Hatua hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam mwaka 1991, kutungwa kwa Sheria ya Usafiri wa Majini ya mwaka 2003 na kanuni zake pamoja na kutungwa kwa Sheria ya Usafiri Baharini ya mwaka 2006 ya Zanzibar na kanuni zake.

 

UNICEF:KUANGAZA UMUHIMU WA MAENDELEO YA WATOTO WADOGO ECD.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF Septemba 22 lilikuwa na tukio maalumu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwaajili ya kuangaza umuhimu wa maendeleo ya watoto wadogo ECD.

Kwa mujibu wa wa shirika hilo lilisema kuwa Elimu ya awali, upendo na lishe bora ni misingi muhimu katika kuhakikisha akili za watoto wadogo zinakuwa vizuri. Akiongea na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Anthony Lake alizingatia umhimu wa kuwapatia watoto wadogo huduma za elimu, lishe bora na kupambana na ukatili dhidi yao kwani alisema

Mtoto akikosa kuchangamshwa ipasavyo anapokuwa mdogo, akili zake hazitakuwa vizuri, kwa sababu kila sekunde, seli elfu moja zinaungana ubongoni mwake. Zisipoungana, utaleta tofauti kubwa sana kwenye maisha ya baadaye ya mtoto. Aidha alieleza kwamba bado watoto milioni 160 duniani kote wamedumaa, ambao hawataweza kuwa na akili na fursa sawa kama wenzao.

Na kwa upande wake Balozi Mwema wa UNICEF mwanamuziki Shakira alisema kuwekeza katika maendeleo ya watoto wadogo kunakuza ukuaji wa uchumi kunapunguza tofauti na kunasaidia kuondoa uhalifu na vurugu. Kwa hiyo kuna ufanisi. Bila shaka ni njia bora kuhakikisha dunia yenye utulivu, amani na maendeleo." Katika hotuba yake wakati wa mkutano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwekeza katika maendeleo ya watoto wadogo hainufaishi tu watoto bali pia jamii kwa ujumla, akifuraishwa kuona kwamba swala hilo limeingizwa kwenye malengo ya maendeleo endelevu.

 

 

 
 








All the contents on this site are copyrighted ©.