2015-09-23 15:36:00

Viongozi wa Bara la Ulaya wakutana Mjini Bruxelles kwa majadiliano ya wakimbizi


Wakati viongozi wa bara la  Ulaya wakikutana mjini Brussels nchi Ubelgiji, 22-23 Septemba , Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNCHR limewataka viongozi hao kuungana dhidi  ya dharuara ya janga la wakimbizi na wahamiaji ambalo linaongeza machafuko yasiyotabirika.

Kwa mjibu wa shirika la wakimbizi (UNHCR), linasema hii ni fursa ya mwisho kwa bara Ulaya kushughulikia janga hili ambalo linaongeza mateso na unyanyasaji kwa wakimbizi na wahamiaji pamoja na kusababisha mivutano baina ya nchi.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa wa UNHCR António Guterres, janga hili ni la utashi wa kisiasa linalotokana na ukosefu wa Umoja baina ya nchi za Ulaya jambo linalosababisha ghasia akitolea mfano wa raia wa Hungary takribani 200,000 waliokimbilia Austria na Yugoslavia mwaka 1956 ambao walipokelewa vizuri na utaratibu wa kuwahamishia wengine 140,000 katika nchi nyingine ulifanyika hima.

Msema ji wa wa shirika la wakimbizi UNHCR Melissa Falaming alisema kuwa wanaamini kwamba katika mipango wanapaswa kuzingatia maelfu ya wakimbizi na wahamiji  wanavyo hitaji malazi na misaada mingine katika maeneo hayo ya kuwapokea kwa wakati.

Aidha i Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuwapa hifadhi wakimbizi laki moja na elfu 20 kwa kipindi cha sasa pekee hautoshi.

Msemaji wa kamisheni hiyo, Melissa Fleming amesema kuwa mpango huo wa Umoja wa Ulaya utakuwa na mwafaka  iwapo utarahisisha kukubaliwa makumi ya maelfu ya wakimbizi katika nyakati nyingine. Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imewataka viongozi wa nchi za Ulaya kukubali na kuunga mkono mpango wa kuwapa hifadhi wakimbizi laki moja elfu 20 ili kuweza kukabiliana na mgogoro wa wahajiri unaoshuhudiwa sasa barani humo.

Maelfu ya wakimbizi hususan kutoka nchi za Syria na Iraq wanaendelea kumiminika katika nchi za Ulaya, suala ambalo limesababisha mgogoro mkubwa katika nchi za bara hususani nchi ya Hungary , Jamhuri ya Cecosvolakia na Romania waliokataa  kupokea a idadi ya wakimbizi katika mpango uliotolewa na Kamishana kuu  Jumanne  Septemba 22 katika Mkutano mkuu huo  huko Bruxelles Ubelgiji.








All the contents on this site are copyrighted ©.