2015-09-22 15:28:00

Papa ahimiza waamini kumfuata Maria katika kukutana na Yesu


 Jumanne majira  ya saa mbili za Asubuhi , Papa aliongoza Ibada ya Misa katika madhabahu ya Mama Yetu wa Upendo wa El Cobre, yaliyoko Santiago.Katika Ibada hii Papa alisistiza jinsi Mungu anvyotutaka sisi kwenda kukuzingatia utamaduni wa kukutana na wengine . Na kwamba Mungu anatutembelea ili nasi twende kuwatembelea wengine, ili kuufikisha upendo wake wa kuokoa kwa wengine pia. 

Papa alieleza hilo , katika homilia yake akifakari juu ya somo la Injili. Alisema somo hili linatutaka siku zote kuuona uwepo wa Mungu katika maisha yetu, maisha yasiyojitenga kamwe na  utulivu wa Mungu , wenye kutusukuma kuwa wema na kuhudumia wengine. Na kwamba, Mungu hututembelea ili nasi  tuweze kuwatembelea wengine, na Mungu hukutana asi ili pia nasi tuweze kukutana na wengine , na tunaupata upendo wake Mungu ili nasi tuweze kuutoa kwa wengine.

Papa alielekeza tafakari yake kwa Bikira Maria , mwanafunzi wa kwanza wa Yesu, Mwanamke kijana mwenye umri mdogo , binti wa kijiji kidogo cha Palestina, aliyetembelewa na Bwana, na kuambiwa atakuwa  mama wa Mwokozi. Maria wakati anatembelewa na Malaika hakuwa na mawazo yoyote juu ya kuwa Mama wa Mwokozi, lakini alisikiliza kwa makini sauti ya Bwana, na  kuitikia huku akiendelea kutumikia familia yake. Na baadaye  aliona haja ya kwenda kumsaidia binamu yake Elizabeth kwa furaha zote. Papa anasema, ndivyo inavyotakiwa pia kwa kila muumini anayetembelewa na Yesu kuwa na furaha ya kwenda kuhudumia wengine walio wahitaji zaidi .  Na ndivyo Maria hata leo , anavyoendelea kutuletea Neno la Mungu , Neno la mwanae , Bwana wetu.

Papa alieleza na kutaja kwamba , katika madhabahu hayo ya el Cobre,  yenye kuwa na kumbukumbu  takatifu ya kutembelewa na Maria, kwa namna ya kipekee anaziunda roho za Wacuba, huvuvia mioyo ya watu wake na upendo mkuu wa Mungu ndani ya familia na taifa kwa ujumla.  Papa Francisko alieleza na kukuumbuka jinsi Papa Benedikto XV, alivyo mtangaza Mama Yetu wa Upendo wa Cobre kuwa Mlinzi wa Cuba. Na njinsi Wacuba wa wakati ule, walivyokuwa na imani imara , wakiandika kwamba wala si umaskini au maafa yanayoweza kuichukua imani yao na upendo wa Wakatoliki kwa Bikira Maria wa Cobre , ambamo waliweka majaribu na furaha yao yote kwa Ua hilo  angavu na faraja kama umande wa asubuhi katika nchi kavu. Maria wa Cobre anayependwa na kuheshimiwa saana na waamini Cuba,  ambao humiminika kwa wingi kila mwaka kufanya hija katika madhabahu hayo

Papa Francisko anasema katika  madhabahu haya tunaweza uona upendo wa Mama Maria kwetu sote.. Na kutoka  katika  madhabahu hayo, kuna mzizi wa utambulisho wetu, tunapata kujua mahali pa kuchota nguvu za kusonga mbele bila kukata tamaa katika kuifuata njia ya ukombozi ya Kristo hata wakati wa shida na dhiki nyingi.

Papa alieleza na  kuziombea roho za watu wa Cuba,kuitikia wito wa Bwana anapowatembelea katika maisha yao ya kila siku. Maisha ya kila siku, Papa alifafanua ni utendaji wote wa nyumbani ,  utendaji unaoweza kupata hisia za uwepo wa Mungu, Baba ambaye humweka mtu huru, na mwenye nguvu za , huponya, msaada  wa ujasiri na mtumishi,kimbilio na ishara ya uhakika ya ufufuo mpya.  Na alikumbusha kwamba , uwepo hai wa Mungu huonekana kupitia njia ya  huduma kwa wengine  na Mungu huonekana katika  unyenyekevu wa mtu.  








All the contents on this site are copyrighted ©.