2015-09-21 14:59:00

Ban Ki-Moon Matumaini ya amani yanaonekana kuwa mbali katika dunia ya sasa


 Matumaini ya amani yaonekana kuwa mbali katika dunia ya sasa iliyokumbwa na mizozo na mapigano, hii ni ndoto zilizo ndani ya maisha ya  watu kila mahali duniani.

Ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa ban Ki- moon aliyoitoa Septemba 21 katika siku ya amani Duniani, Ban Ki-moon alisema hakuna kundi linaloweza kufanikisha kufikia ndoto hiyo ya amani zaidi ya vijana ambao alisema kwa sasa ni wengi na hivyo,  Viongozi hawana budi  kuwekeza kwa vijana katika ujenzi wa amani. Aidha alisema sote tunaweza kuimarisha amani, Mashirika ya kiraia, kampuni na hata taasisi za kidini wote wanaweza kujenga dunia yenye amani zaidi.

Aliendela kusema kwamba ubia huo katika ujenzi wa amani ndio msingi wa ujumbe wa siku ya amani mwaka huu na kauli ya mbiu isemayo “ubia kwa amani utu kwa wote”

Katibu Mkuu amesema zama za sasa  i ni za vitisho lakini pia ni zama za matumaini makubwa kwani siku chache viongozi wa dunia watakutana Umoja wa Mataifa kuridhia ajenda 2030 ambayo amesema ni hatua ya msingi inayoashiria maisha yenye utu kwa wote, ambako umaskini utasalia historia  amani itatamalaki.

 Katika kilele cha siku hiyo Katibu Mkuu Ban Ki - moon aliongoza shughuli ya kugonga kengele ya amani kwenye bustani ya Umoja wa mataifa mjini New York Marekani,  ikiwa ni ishara ya kuadhimisha siku hiyo ya amani.

Wakati huo huo malengo ya maendeleo endelevu, SDG au ajenda 2030 ikitarajiwa kuridhiwa na wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wiki ijayo mjini New York,

Marekani bado inatafuta mbinu ya  jinsi ya kupata mabilioni ya fedha ya kugharamia malengo hayo.

Njia mojawapo inayoangaziwa ni kuhamasisha uwekezaji wa sekta ya kibinafsi katika kujenga miundombinu, barabara, daraja na mabwawa, ambayo yatahakikisha kuwa nchi zinaweza kukua bila kufilisisha serikali.

Ni kwa mantiki hiyo tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Ulaya, UNECE imeandaa maonyesho huko Geneva, Uswisi kudhirisha jinsi ubia kati ya serikali na sekta binafsi, PPP unaweza kufanikisha malengo hayo.

Imetolea mfano mradi wa aina hiyo huko Belarus wa ujenzi wa barabara kubwa ya kuunganisha nchi za Muungano wa Ulaya na Asia ukiwa na  thamani ya dola Milioni 350, mradi ambao unaelezwa utainua uchumi wa nchi husika.(Chanzo :Kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa)

 








All the contents on this site are copyrighted ©.