2015-09-20 08:48:00

Papa asema ni kujenga upya ushirikiano na urafiki na kuwatia moyo watu wa Quba


Vatican Radio: Papa alianza na shukrani kwa rais, viongozi wa nchi na Maaskofu na kwa watu wote kwa mapaokezi yao na shukrani kwa maneno ya hotuba ya rais kwa niaba ya serikali na ya watu wote wa Quba.

Vilevile shukrani kwa Kardianali Jaime Ortega  Alamino Askofu Mkuu wa Habana ,Rais wa Baraza la maaskofu wa Quba Dionisio Guillermo García Ibáñez Askofu Mkuu wa Santiago ya Quba. Na maaskofu wote pamoja  na watu wote wa Quba kwa makaribisho hayo.

Hakusahau kuwashukuru wote  kamati ya maandalizi kwa kufanikisha  safari ya kitume na kumuomba Rais amfikishie salam zake za kipekeekwa rais mstaafu Fidel , vilevile kwa wote amabao kwa sabbu moja au nyingine hawataweza kukuatana na papa katka ziara hiyo.

Papa alisema mwaka huu 2015  unaangukia katika mwaka wa nane katika ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Jamuhuri ya Quba na ya Vatican .Ni wadhifa mkubwa kuweza kufika katika nchi  hiyo ambayo tayari ilishatanguliawa na mapapa wenzake kwa safari za kitume ambayo  hazitasauhulika za Papa Yohane Paulo wa Pili na Benedict  wa kumi na sita.

Papa alisema anatambua vema ni jinsi gani  safari zao ziliacha kumbukumbu kwa watu na viongozi wa kisiwa cha Quba. Na kusema leo tunajenga kwa upya ushirikiano na urafiki ambao Kanisa inaweza kuendeleza na kuwatia moyo watu wa Quba kwa matumaini yao, na kwamba wanaweza kuelekea katika  njia uhuru na nafasi zinazohitajika kutangaza ufalme hasa kwa watu walioko pembezoni mwa jamii.

Safari yake hiyo pia inaangukia katika sherehe za 100 za kutangazwa Mama Maria wa Upendo huko Cobre kuwa msimamizi wa kisiwa cha Quba .Papa aliendelea, walikuwa ni maveterani kutafuta huru , ambao waliongozwa na imani na ya uzalendo wakamuomba Bikira wa Quba (Mambisa) awe ndiye msimamzi wa nchi huru na ya utawala. Yeye aliwasindikiza katika historia ya watu wa Quba akiwatia matumaini,  pia anawalinda katika utu wa watu kwenye maisha yao magumu , na kuwatete kwa kila hali katika utetezi kama wanadamu.

Papa aliendelea kusema ya kwamba uzoefu huo unazidi kukua kwa bikira wa upendo wa Cobre ambao ni ushuhuda unaonekana katika mioyo ya watu wa Quba. Aliongeza ya kwamba katika ziara yake , atakuwa na fursa ya kwenda kwenye madhabau ya Cobre kama mtoto anayekwenda kuhiji, asali kwaajili ya watu wote na  watoto wa Quba, amabao ni wapendwa wa Taifa kwa mama Maria ili wapate kutembea njia ya haki, amani, uhuru na mshikamano.

Papa alisema kwamba kijiografia Quba ni kisiwa kinachounganisha njia zote , kikiwa na thamani kama ufunguo kati ya  kaskazini na kusini, ,mashariki na magharibi.Wito wake wa asili ni ule wa kuwa kutuo cha kukutana kwasababu watu wote ufanya makutano katika urafiki kama ilivyokuwa ndoto ya shujaa wao Jose Marti “zaidi ya vikwazo vya shingo na vikwazo wa bahari” vilevile katika maneno ya papa Yoahane Paulo wa Pili alipotembelea Quba 1998 akisema ili Quba ipate kufungua uwezekano wa ajabu katika ulimwengu na pia ulimwengu ujifungue kwa quba. (Ujumbe wa,Januari  21,  1998, 5).

 








All the contents on this site are copyrighted ©.