Kamati ndogo ya Tume ya Mawasiliano na Matangazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, imetoa baadhi ya mikakati mbinu, kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Papa Francisko nchini Kenya, mwezi Novemba mwaka huu.
Akizungumza na AMECEA Online News, Mratibu wa Mawasiliano wa KCCB, David Omwoyo amesema kuwa tovuti maalum kwa ajili ya ziara ya Papa itazinduliwa katika siku chache zijazo. Na pia hivi karibuni , nembo ya ziara ya Papa itazinduliwa hivi karibuni. Nembo hiyo ina alama 4 muhimu zinaashiria mada mbiu ya ziara : "Simama imara katika Imani ... Usiogope". Vitu hivyo vinne ni Njiwa kama alama ya amani, moto katika nafasi ya Roho Mtakatifu , ramani ya Kenya na Msalaba ambayo ni ishara ya Kanisa.
Na kwamba, kwa ajili ya kuwaandaa watu , katika kipindi hiki cha kusubiri ujio
wa Papa , Kamati ndogo ya Mawasiliano imeunda mpango mpya wa utendaji kwa miradi
maalum, inayolenga kufanikishaji wa ziara ya Papa kiroho na kijamii. Miradi inayoendeshwa
na Kanisa Katoliki Kenya ambayo itatagazwa kupitia vituo vya Televisheni . Na Kutakuwa
na mengi yatakayotangazwa na vyombo vya habari kwa wakati huu. Na kwamba, Taarifa
zote zitakuwa zinapatikana katika tovuti mpya itakayozinduliwa hivi karibuni, ikiwa
wazi kwa mtu yeyote ambaye anayetaka kupata habarii za ujio wa Papa Kenya. Papa Francisko
anatazamia kutembelea Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika Kati , mwezi Novemba mwaka
huu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |