2015-09-18 15:08:00

Kanisa lituhumiwa kuhusika na uwepo wa ufisadi na rushwa Liberia


Wafanyakazi serikali ni watu wa kawaida wengi wao wakiwa wafuasi wa Makanisa mbalimbali . Na hivyo utendaji wa watu hao unaonyesha jinsi walivyolelewa. Kama hawakulelewa vyema kuzingatia uadilifu na uaminifu, ni wazi itakuwa vigumu kwao kukataa tamaa na vishawishi vya rushwa na ufisadi. Ni maoni ya Waziri wa Habari Lewis Brown na Naibu Waziri Isaac Jackson walipo zungumza na wanahabari siku ya Jumanne, kama kujibu tuhuma zilizotolewa na Baraza la Makanisa juu ya ufisadi na utawala mbaya wa serikali nchini Liberia. 

Tamko la LLC la hivi karibuni linasema serikali ya Liberia inapalilia rushwa na ufisadinakusaba bisha umaskini wa kukithiri kwa wengine. Na  pia Kanisa limeikosoa sekta ya afya na elimu, kwamba katika siku za hivi karibuni hakuna mipango yoyote ya kimaendeleo inayoendeshwa katika sekta hizo.  

Naibu Waziri Jackson, akitoa jibu kwa tuhuma hizo alirudisha mpira wa lawama  kwa Kanisa akisema  wale wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi na wala rushwa ni waamini wa makanisa mbalimbali nchini humo. Wafanyakazi wengi wa serikali ni waamini wa Makanisa, je kulikoni Kanisa liilamu serikali? Kumbe wa kulaumiwa ni Kanisa lenyewe kwa kutokuwa na majiundo thabiti ya tabia za waamini wake katika maisha ya kijamii. Kutokana na ulegevu huo, watu wake hawaoni kama rushwa na ufisadi ni dhambi. Hivyo uzembe wa Kanisa katika malezi ndiyo unapaswa kulaumiwa kwa kusababisha uwepo wa rushwana ufisadi kwa wafuasi wa Makanisa. 

Naibu  Waziri anasema, badala ya kutuhumiana ni vyema kanisa na serikali kufanya kazi kwa  kushirikiana, katika kupambana na rushwa  kupitia  njia za kujenga maisha matakatifu na aminifu miongoni mwa watu.  








All the contents on this site are copyrighted ©.