2015-09-14 08:05:00

Papa - Benki za maendeleo Vijijini tendeni kwa uaminifu na ubunifu zaidi


Baba Mtakatifu Francisko, ameutaka uongozi na wafanyakazi wa Benki za maendeleo vijijini,  kutenda kwa moyo wa uaminifu na ubunifu zaidi katika kazi yao ya kibenki , ili watu wengi zaidi waweze kunufaika na huduma ya Benki.  Papa alileleza hilo, siku ya Jumamosi wakati akikutana na kikundi cha uongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Benki ya Mikopo ya Ushirika ya Roma(BCC), ambao walikuwa na Mkutano wao Mkuu wa 60.  

Baba Mtakatifu alionyesha hisia zake kwamba, katika  asili ya benki ya vijijini, inatarajiwa kwamba,  chama cha mikopo, kinaweza kuchochea mipango mingine ushirikiano. Na wazo hilo linaendelea kuwa la thamani kubwa. Hivyo  BCC inaweza kuwa chimbuko la ujenzi wa mtandao mkubwa, wenye  kuzaa matawi mengine yanayoweza saidia kutoa ajira  na kusaidia familia, kupitia uzoefu wake katika utoaji wa mikopo midogo midogo na njia nyingine za kukuza uchumi.

Papa alieleza na kuhimiza Benki hiyo ya Mikopo ya ushirika, kutenda kwa  ukarimu zaidi katika maisha na harakati za  vyama vya ushirika, akitolea mfano wa  BCC ya  Roma, ambayo kwa sasa ina matawi yake hata nje ya Roma mkoani Lazio na Abruzzo. Na kwamba kutoka maeneo wanayoendesha sasa wanaweza kupanua zaidi shughuli zao kwa moyo wa uaminifu na ubunifu zaidi katika kueneza moyo wa ushirika wa vyama vya mikopo. 

Hotuba ya Papa ilirejea ufahamu wa Kanisa juu ya manufaa watu kuunganisha nguvu na kujenga ushirika  kama kigezo  muhimu na chenye thamani kubwa katika kuleta ustawi wa jamii mahalia. Kama ilivyokuwa kwa Mapadre walioweka imani yao katika ushirika, wakihamasishwa na moyo  wa mshikamano wa Kikristo, walianza juhudi za maendeleo kwa kutumia nguvu ya ushirika.

Papa alieleza na kuhimiza mambo kadhaa ambayo tayari aliyatoa pia katika mkutano mwingine wa Muungano wa Mashirikisho ya hapa Italia kwamba,  ni kuendelea kuwa injini ya maendeleo hasa kwa maeneo yanayokaliwa na jamii dhaifu ya jamii na vyama vya kiraia, na hasa katika kuwawezesha vijana wasiokuwa na ajira, na kuhimiza mijadala ya kuanzishwa kwa makampuni mapya  na vyama vya ushirika.

Papa amewahimiza viongozi wakuu wa vyama vya ushirika kwamba , daima ni lazima wawe mstari wa mbele kupendekeza na kutekeleza ufumbuzi mpya wa jamii na hasa katika masuala yanayohusiana na afya.
- kuonyesha kujali  uhusiano kati ya uchumi na haki za kijamii na kudumisha a hadhi na thamani ya utu wa mtu.
- Kuhamasisha na kuwezesha maisha chanya katika familia, hasa kupitia uundaji wa usimamizi wa masoko kwa bidhaa za kawaida zinazozalishwa  na ushirika.

-Aidha ni muhimu kwao kukuza matumizi bora ya fedha katika vyama vya ushirika, ili kweli manufaa ya ushirika iwe ni wote na hatimaye wote washiriki kwa kikamilifu katika mfumo wa  utandawazi, kwa sababu utandawazi ni mshikamano wa jamii . 








All the contents on this site are copyrighted ©.