2015-09-11 08:22:00

Papa akutana na Waziri Mkuu wa Kuwait


(Vatican Radio)  Jumatano, Septemba 10, 2015, Papa Francis alimpokea na kuzungumza nae , Waziri Mkuu wa Kuwait, Sheikh Jaber Mubarak Al-Hamad Al-Sabah. 

Katika mazungumzo yao ya kirafiki , waligusia mandhari mbalimbali ya maslahi kwa pande zote ikiwemo  michango chanya ya kihistoria ya Wakristo wachache miongoni mwa jamii Kuwait. Na pia walilenga umuhimu wa elimu katika kukuza utamaduni wa kuheshimiana,  mshikamano na ujenzi wa amani kati ya watu tofauti na wenye dini tofauti.

Baada ya Kukutana na Papa,  Waziri Mkuu Sheikh Jaber na ujumbe wake alikutana na Katibu wa Nchi wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin,akiwa amefuatana Askofu Mkuu Paulo Ghallager , Mkuu wa Idara ya mahusiano ya nchi za nje wa Vatican. Lengo la kukutana kwao ilikuwa  kutia saini katika Mkataba wa Maridhiano kati Sekretarieti ya Nchi  ya Vatican na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi ya Kuwait . Utiaji huo wa saini,  ulifanywa na  Askofu Mkuu Paulo Gallagher na Waziri  Sheikh Sabah Khalid Al-Hamad Al-Sabah, Naibu Waziri katika  waziri wa Mambo ya Nje, Kuwait.

Taarifa inataja kuwa Mkataba huo,  unawezesha utendaji thabiti zaidi kwa pande zote mbili, kuimarishwa  zaidi na kuwa na mahusiano thabiti baina ya nchi, katika kushirikiana , kuheshimiana, kujenga  amani na utulivu wa kikanda na kimataifa.








All the contents on this site are copyrighted ©.