2015-09-11 11:54:00

Hakuna mbadiliko katika sheria msingi ya ndoa.


(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko wiki hii alitoa nyaraka mbili za “Motu proprio”zinazolenga kufanya mabadiliko katika Mfumo wa Mahakama ya Kanisa Katoliki juu ya uendeshaji wa kesi zinazohusiana na sheria ya ndoa.

Papa alitoa nyaraka hizo siku ya Jumanne, Motu proprio,  “Mitis Iudex Dominus Jesus”au Bwana Yesu, Hakimu mwenye huruma", ambayo inarekebisha kanuni za mahakama ya sheria ya kanisa (CIC) kwa Makanisa ya Amerika, na barua nyingine, “mitis et misericors Jesus"Msamaha na huruma  ya Yesu”, ambayo inafanya inarekebisha Kanuni za Makanisa  za Kanisa katika uendeshaji wa kesi za kubatilisha ndoa kwa Makanisa ya Mashariki (CCEO).

Profesa katika Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa ya Gregorian Rome, Padre James Conn, SJ, akizungumzia  marekebisho hayo ameiambia Redio Vatican kwamba,  kuna mabadiliko maalum matatu , hasa katika uharakisha wa kushughulikia  kesi za wanaondoa wanaotaka kubatilisha ndoa;  kuondolewa kwa haja ya mahakama kutoa hukumu mara mbili kwa tukio na kisha tena kupelekwa katika mahakama ya rufaa, kwa maana kwamba, inatosha kuzingatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa mara ya kwanza, iwapo  yanayoona kwamba , kuna ushahidi wa kutosha kwa ndoa kutanguliwa, na wahusika wanaweza kufunga ndoa   ndoa mpya kwa mujibu wa sheria Kanisa (au katika kupokea miungano ya ndoa ilifungwa  kwa sheria za kiraia , wakati huo huo kutambuliwa na Kanisa).  

Pia kuanzishwa kwa uwezekano wa kesi kusikilizwa na hakimu mwenye uzoefu mara  moja, kama hatua ya kupunguza mzigo wa wingi wa kesi katika mahakama za majimbo, ambako watu wenye ujuzi ni wachache);  Na uundaji wa kueleka mchakato wa kesi  katika baadhi ya kesi , kutolewa maamuzi moja kwa moja na Askofu mahalia, kwa kesi ambazo zina ushahidi wa kutosha kutolewa hukumu ya kubatishwa na pande zote mbili zinaamini muungano wao ulikuwa batili. Katika mchakato huu hasa unaonyesha dhamira Papa Francisco  kugawana madaraka na Maaskofu wa majimbo duniani kote.

Prof Conn, SJ, aliendelea kufafanua kwamba - kinyume na uvumi uliotolewa na baadhi ya vyombo vya hata katika vyombo vya Kanisa, mabadiliko yamefanyika katika misingi ya uelewa wa Kanisa la asili na muundo wa kimsingi wa ndoa, na hivyo hakuna mabadiliko kaika Madhumuni msingi na katika  wigo wa mfumo wa Mahakama wa Kanisa. Na wala hakuna mabadiliko katika mafundisho ya Kanisa  juu ya kutengua ndoa, alisema Prof. Conn, SJ. Na kwamba, nyaraka mpya za mabadiliko hazibadilishi kanuni zinazofuatwa na Mahakimu katika  kubatilisha ndoa  na wala hazibadili uhalali wa ndoa,  hivyo, ndoa kubatilishwa linabaki ni jambo linalohitaji uwepo wa ushahidi wa kutosha . 








All the contents on this site are copyrighted ©.