2015-09-10 15:58:00

Tanzania, Wanafunzi wa Darasa la Saba wamefanya Mtihani wa Taifa


Rais Jakaya  Kikwete alitoa kauli juu ya madai kuwa elimu inayotolewa Tanzania ni duni, na potofu kana siyo kweli  kwani wahitimu wake wanakubalika duniani.

Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete alisema tatizo liko kwenye kuwaandaa wahitimu kukidhi matakwa ya soko la ajira la ndani na la kimataifa.  “Elimu yetu ni bora na inakubalika popote duniani...wahitimu wanaweza kufanya kazi katika nchi yoyote, kinachotakiwa ni kuwapatia ujuzi wa kutosha kukidhi matakwa ya soko la ajira,” alisisitiza Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo.

 Takwimu zinaonyesha kwamba vijana wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka nchini ni kati ya 800,000 hadi milioni moja na wanapigania nafasi za ajira zisizozidi 60,000 katika sekta ya umma na nafasi takribani 300,000 katika sekta binafsi.

Rais Kikwete alisema serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuvutia wawekezaji na kuomba mchango wa kila mdau kutumia fursa na rasilimali zilizopo nchini kuzalisha mali na kuongeza ajira katika sekta ya umma na sekta binafsi.

 Wakati huo  wanafunzi wa darasa la saba nchini kote jumatano 9 Septemba Jumla ya watahiniwa 775,729 walitafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, mtihani wa siku mbili na  kushirikisha shule za msingi 16,096 nchini kote. Inasemakeana ya kuwa mtihani huo wa kitaifa ulifanyika katika mazingira ya amani na utulivu .

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 8Septemba, Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk. Charles Msonde, alisema masomo yatakayotahiniwa ni matano ambayo ni Kiswahili, Kingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.

“Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE)  katika shule 16,096 za msingi, huku watahiniwa waliondikishwa kufanya mtihani huo ni 775,729 kati yao wavulana 361,502 sawa na asilimia 46.6 na wasichana 414,227sawa na asilimia 53.4,” alisema

Dk. Msonde alisema jumla ya watahiniwa 748,514 watafanya mtihani kwa Kiswahili na watahiniwa 27,215 watafanya wa Kiingereza ambazo ni lugha walizokuwa  wakitumia katika kujifunza.

 Alisema kati ya watainiwa hao, wasioona ni 76 wakiwamo wavulana 49 na wasichana 27 na watainiwa wenye kuona  hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 698 kati yao wavulana ni 330 na wasichana 368.

Alitoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo pamoja na kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani kuwa salama, tulivu na kuzuia mianya inayoweza kusababisha udanganyifu.

 Pia aliwataka wasimamizi wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani Necta itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya taifa.

Na Walemavu wa macho watapiga  kura wenyewe:

Taarifa zinasema kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, watu wenye ulemavu wa macho watashiriki katika kumchagua kiongozi wanayemtaka kwa kutumia kifaa maalum chenye maandishi ya nukta nundu au Braille katika uchaguzi mkuu utakofanyika Oktoba 25 waka huu.

Vifaa hivyo vitaanza kufanyiwa majaribio mwishoni mwa mwezi huu ambapo watu hao wataweza kufundishwa jinsi ya kupiga kura bila ya kuwa na mtu wa kumsaidia au kumwongoza kupiga. Kumekuwa na madai kuwa wale waliokuwa wakiwasaidia watu wenye ulemavu wa kuona mara nyingi huwapotosha walemavu hao kwa kupiga kura kinyume ya matarajio ya mlemavu huyo.

Tangu jadi walemavu wa macho wamekuwa wakishiriki katika kupiga kura kwa kusaidiwa na watu ambao huwa wakwenda nao katika vituo vya wa kupiga kura kwa lengo la kuwaelekeza wakati mwingine husaidiwa na mawakala au wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.