2015-09-09 14:59:00

Kateksi ya Papa yahimiza :familia na makanisa lazima kuwa wazi,


(Vatican Radio) Papa Francisko katika Katekesi yake ya  Jumatano ameendelea kuzungumzia juu ya familia, akipeleka mawazo yake juu ya uhusiano uliopo kati ya kati ya familia na jumuiya ya Kikristo.

Papa Francisko amebainisha kuwa dhamana kati ya familia na jumuiya ya kikristo,  ni dhamana asilia  kwa sababu, Kanisa ni familia ya kiroho, na familia ni Kanisa kidogo. Kanisa, ni nyumba ya walio amini katika Yesu kama chanzo cha udugu na mshikamano kati ya watu wote. Matukio makubwa ya nguvu kidunia yaliyoandikwa katika vitabu vya historia, yamebaki hivyo katika vitabu , lakini historia ya  upendo wa binadamu,  imeandikwa moja kwa moja kwenye moyo wa Mungu, na kwamba ni utendaji unaobaki kuwepo milele yote. Na hii ndiyo maana alisisitiza Papa,  kwa nini familia ni muhimu sana.

Aliendelea kuyatazama maisha ya Yesu mwenyewe kwamba,  baada ya kuishi kwa miaka thelathini ndani ya familia,  Nazareti, aliwakusanyika jamii waliokuwa wamemzunguka, na kuunda Kanisa.  Na familia hii, Papa amesema,  si familia iliyofungwa na mipaka ya kimadhehebu au itikadi lakini familia yenye kukaribisha wote, kama ilivyokuwa kwa familia ya Yesu, haikuwa tu ya mitume , lakini pia waliwakaribisha wenye njaa na kiu, wageni na wateswa, wenye dhambi na Mafarisayo.

Kwa sababu hii, Papa Francis amesema kuwa linakuwa ni jambo muhimu kwa ajili ya  kuimarisha mapatano kati ya familia na jumuiya ya Kikristo.  Aliendelea kusema kwa kuitazama familia katika mapana ya mkusanyiko wa familia nyingi pamoja chini ya jina Parokia, na kusema kwamba, familia na Parokia, yanakuwa ni maeneo mawili,  jumuiya ya upendo inayotembea katika barabara ambayo , chanzo chake  na mwisho ni Mungu mwenyewe. "Baba Mtakatifu amesema, waamini wa Kristo wanahitaji kupata uelewa na ujasiri wa kufanya upya ahadi yao ya  imani na ukarimu.  Hivyo ni kwa njia ya neema ya Mungu, jamii  na parokia, zinaweza kuwa uwezo wa kukamilisha "muujiza" wa kuchagiza udugu zaidi kama ilivyokuwa kwa kanisa la mwanzo duniani.








All the contents on this site are copyrighted ©.