2015-09-07 16:16:00

Papa Francisko asema Wakristo wanaendelea kuteseka kimyakimya


Jumatatu hii 7 Septemba katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican, wakati wa Ibada ya Misa ya mapema asubuhi, Baba Mtakatifu Francisco, aliongoza Ibada ya Misa akishirikiana na  Patriaki wa Cilicia ya Armenia, aliyechaguliwa hivi karibuni, Mwenye Heri Gregory Petro XX. Katika Ibada hiyo, wakiwepo pia Maaskofu wa Sinodi ya Kitume ya Armenia ya Kanisa Katoliki, na Kardinali Leonardo Sandri, Mkuu wa Usharika kwa ajili ya Makanisa Katoliki ya Mashariki.

Papa katika homilia yake baada ya masomo ya siku alivyozungumzia jinsi leo hii Wakristo wengi, wanavyoendelea kuteseka katika maeneo mengi, na huku viongozi wenye mamlaka duniani, wakikalia kimya uhalifu huo. Amesema hata leo hii pengine hata zaidi ya siku za nyuma , Wakristo wanateseka kuuawa au kufukuzwa katika nchi zao kwa sababu tu ya imani yao kwa Kristo.

Papa kwa uchungu, amewatia moyo Wakristo akisema, ndugu zangu wapendwa kwa hakika hakuna Ukristo usioandamana na mateso. Na alieleza na kukumbusha juu ya Heri” Heri yenu ninyi watu wakiwatukana , wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu juu yangu ,furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni”. Leo hii hilo linatokea mbele ya dunia na viongozi wameshindwa kusitisha uovu huo.  Wakristo wanapita katika kipindi kigumu cha njia ya mateso , kama ilivyokuwa kwa Kristo mwenyewe.   

Papa alieleza na kukumbuka Madhulumu haya kwa Wakristo, Taifa la Armenia likiwa moja ya Mataifa ambako Wakristo wengi waliipita njia hii ya mateso.  Taifa la kwanza kuongokea Ukristo. Papa alieleza na kuwakumbuka pia Wakristo wa Libya, Misri, Iraki  wanaochinjwa kama kuku kwa kuitangaza Injili ya Kristo. 

Papa amesali ili Bwana leo hii aweze kutufanya sisi sote kusikia ndani ya mwili wake Kanisa, upendo mkuu kwa ajili ya wafia dini wa wakati wetu na pia katika kuwa tayari kufa kifo dini. Na kwamba , hakuna Mkristo mwenye kujua hatima ya maisha yake mbele ya uso huu wa madhulumu. Na hivyo ni vyema kuiomba neema ya Bwana ili kama hili litatokea siku moja , tuwe na ushupavu wa kutoa ushahidi wetu  kama wafia dini wengine walivyotuonyesha. Na hasa Wakristo wa Armenia.  

Papa Francisko  awali alitoa  barua  kwa Patriaki mpya wa  Cicilia ya Armenia, ambayo ni tahafifu mpya kwa ajili ya  ushirikiano na Makanisa ya  Mashariki, barua ya tarehe  25 Julai 2015. Aidha taarifa za awali zinaeleza, kabla ya Ibada ya Misa , viongozi hawa wawili, walipata nafasi ya kubadilishana zawadi, tukio linalotajwa kuwa ni ishara ya wazi ya umoja wa kikanisa unaoridhiwa na  Baba Mtakatifu Francisko   na Mwenye Heri Gregorio Pietro Ghabroyan , Patriaki wa Cecilia ya Armenia.  Imetajwa hizi ni hisia wazi na ukweli hai wenye kuhamasishwa na Upendo wa Kikristo. 








All the contents on this site are copyrighted ©.