2015-09-01 08:17:00

Farijianeni ninyi kwa ninyi kwa maneno na matendo mema, wala siyo porojo


Tarehe 1 Septemba Baba mtakatifu Francis ameanza maadhimisho ya misa ya kila Siku katika Kanisa dogo  la Mtakatifu  Marta mjini Vatican baada ya kusitisha karibia kwa kipindi cha miezi miwili.

katika mahubiri yake amegusia juu nguvu ya mkristo anaiyopata kutoka kwa Yesu mwenyewe, kwasababu matumaini ya kukutana na Yesu mwishoni inakufanya utie   juhudi kati ya wakristo wenyewe kwa wenyewe katika  kufarijiana  kwa maneno mema na matendo , na wala siyo porojo zisizo faa .

Aliyasema hayo akichambua  jumuiya ya kale ya Watesalonike katika somo la liturjia ya siku ambapo Mtakatifu Paulo alikuwa akiwaelekeza kutokana na mahangaiko ya maswali mengi juu ya ujio wa Yesu, hadi kufikia kukaa bila kazi, na mtakatifu Paulo akawahasa yakuwa asiyefanya kazi na hasile

Mtakatifu Paulo anaeleza ya kuwa siku ya Bwana itakuja kwa ghafla , kama vile mwizi,pia anaongeza Yesu atakuja kuleta wokovu  kwa yule  anaye mwamini; kwahiyo alitoa wito wa kufarijiana mmoja kwa mwingine.Papa aliongeza , hiyo ndiyo faraja ambayo inaleta matumaini.

 Aidha aliendelea ; huo ndiyo ushauri wa kufarijiana, mmoja kwa mwingine, Vilevile papa aliuliza maswali;  je wote tunafanya hivyo kusubiri ujio wa Bwana ambaye atakuja kukutana nasi?  au ni kuongelea juu ya mambo mengi na hata ya teolojia , mambo ya kanisa, ya mapadre ya  watawa , ya munsinyo na yote hayo , je  Ndiyo faraja ya  matumaini yetu?

Papa alikazia , farijianeni katika Jumuiya na katika maparokia, lakini je ujio wa Bwana unaongelewa katika maparokia na katika jumuiya zetu au ni kupiga porojo za hiki na kile kwaajili ya kupitisha wakati?

Papa alikumbusha  kiitikio cha zaburi "nina uhakika wa kuuona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai. Je una uhakika wa kutafakari wema wa Bwana? 

Lakini upo Mmano wa kuigwa wa  Ayubu pamoja na matukio yake aliyoyapata , yeye  aliweza  kutamka  ya kuwa "ninatambua ya kuwa  Mungu yu hai, nitamwona, na kwa macho  yangu haya  nitamwona". 

Papa alisema ni ndiyo hakika Yeye atakuja kuhukumu , na tunapokwenda kwenye Kanisa la makumbusho la Sistina  upo mchoro mzuri sana  wa hukumu ya mwisho ni wa kweli , lakini je tunafikiria juu ya ujio wake ambapo atatukuja,  na sisi tutamwona kwa macho yetu , tutamkubatia daima. Ndiyo matumaini ya Mtume Paulo anayotuleza kufarijiana  kwa matendo mema , na  kwa manufaa ya kila mmoja

Alimalizia akisema ,tuombe neema hii ya kwamba mbegu iliyo pandwa mioyoni mwetu ikue na hatimaye ipate kukutana na Yeye .








All the contents on this site are copyrighted ©.